Na BENJAMIN MASESE-MISUNGWI
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Amour Hamad Amour, amezindua na kuweka jiwe la msindi katika miradi nane ya maendeleo Wilaya ya Misungwi mkaoni Mwanza yenye thamani bilioni 2.2.
Pia amempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuwaamini na kumuomba kuendelea kuwapa vijana nyadhifa za kuwatumikia Watanzania kwa kuwa ameshuhudia umahiri wao wa utendaji na usimamizi wa miradi katika mikoa, wilaya na halmashauri alizopita hadi sasa.
Kauli hiyo aliitoa juzi wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Misungwi,baada ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi nane ikiwamo ya kiwanda cha kuchakata gesi ya matumizi ya nyumbani, ufunguzi wa shule ya Rishor, klabu ya wanafunzi ya kupinga rushwa na barabara ua Lubuga-Mwaniko hadi Mondo.
Miradi mingine ni ufunguzi wa Zahanati ya Nyangh’omango, Shamba la kuku la Prime Farm Ltd, matanki ya maji katika Shule ya Maalumu ya Msingi ya Mtindo, maabara ya kompyuta katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi-Misungwi na kushiriki katika shughuli za kuwakabidhi mikopo kwa vijana huku akisusia kugawa vyandarua kwa wajawazito.
Alisema katika sehemu alizopita ambazo zinaongoozwa na vijana, ameshuhudia miradi yao ikiwa na ubora, haina ubabaishaji na wanawajibika kama Serikali ya awamu ya tano inavyotaka huku akisisitiza kwamba ikiwa Rais Dk. Magufuli atahitaji kuwajua atamdokeza.
Hata hivyo alidokeza wachache kwamba amekoshwa na utendaji wa Mkuu wa Taasisi ya ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma pamoja, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi na mkurugenzi wake wa halmashauri hiyo.
“Nimeshuhudia kwa vitendo katika maeneo niliyopita kwamba Rais wetu Dk. Magufuli hajakosea kuwateua vijana na kuwapa nafasi, utendaji wao katika miradi waliyoisimamia haina shaka yoyote wanafanya kazi kama serikali ya awamu ya tano inavyotaka.
Hata hivyo walipongeza mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda na Mkurugenzi wake, Eliurd Mwaiteleke kwa jinsi walivyofanikisha sera ya Tanzania ya viwanda inaendelewa kufanikiwa ambapo aliwataka misitu na mazingira kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi juu ya ujio wa gesi na athari za uharibifu wa mazingira.
Katika kutembelea miradi hiyo, Amour alisusia kugawa vyandarua kwa wajawazito katika zahanati ya Nyangh’omango baada ya uongozi wa zahanati hiyo kukiuka taratibu huku akilazimika kufanya kikao cha dharula na mganga mkuu wa wilaya.