24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MIRADI YA SH BILIONI 2.2/- YAZINDULIWA

Na BENJAMIN MASESE-MISUNGWI

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Amour Hamad Amour, amezindua na kuweka jiwe la msindi katika  miradi nane ya  maendeleo Wilaya ya Misungwi mkaoni Mwanza yenye thamani  bilioni 2.2.

Pia amempongeza  Rais Dk. John Magufuli kwa kuwaamini  na kumuomba kuendelea kuwapa vijana  nyadhifa  za kuwatumikia Watanzania kwa kuwa ameshuhudia umahiri wao wa utendaji na usimamizi wa miradi katika  mikoa, wilaya na halmashauri alizopita hadi sasa.

Kauli hiyo aliitoa juzi wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Misungwi,baada ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi nane  ikiwamo ya kiwanda cha kuchakata  gesi ya matumizi ya nyumbani, ufunguzi wa shule ya Rishor, klabu ya wanafunzi ya kupinga rushwa na barabara ua Lubuga-Mwaniko hadi Mondo.

Miradi mingine ni ufunguzi wa Zahanati ya Nyangh’omango, Shamba la kuku la Prime Farm Ltd, matanki ya maji katika Shule ya Maalumu ya Msingi ya Mtindo, maabara ya kompyuta katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi-Misungwi na kushiriki katika shughuli za kuwakabidhi  mikopo kwa vijana huku akisusia kugawa vyandarua kwa wajawazito.

Alisema katika sehemu alizopita ambazo zinaongoozwa na vijana, ameshuhudia miradi yao ikiwa na ubora, haina ubabaishaji na wanawajibika kama Serikali ya awamu ya tano inavyotaka huku akisisitiza kwamba ikiwa Rais Dk. Magufuli atahitaji kuwajua atamdokeza.

Hata hivyo alidokeza wachache kwamba amekoshwa na utendaji wa Mkuu wa Taasisi ya  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma pamoja, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi na mkurugenzi wake wa halmashauri hiyo.

“Nimeshuhudia  kwa vitendo  katika maeneo niliyopita kwamba Rais  wetu Dk. Magufuli hajakosea kuwateua vijana na kuwapa nafasi, utendaji wao katika  miradi waliyoisimamia  haina shaka yoyote  wanafanya kazi kama serikali ya awamu ya tano inavyotaka.

Hata hivyo walipongeza mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda na Mkurugenzi wake, Eliurd Mwaiteleke kwa  jinsi walivyofanikisha  sera ya Tanzania  ya viwanda  inaendelewa kufanikiwa ambapo aliwataka misitu na mazingira kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi juu ya ujio wa gesi na athari za uharibifu wa mazingira.

Katika  kutembelea miradi hiyo, Amour alisusia kugawa vyandarua kwa wajawazito katika zahanati ya Nyangh’omango baada ya uongozi wa zahanati hiyo kukiuka taratibu huku akilazimika kufanya kikao cha dharula na mganga mkuu wa wilaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles