30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WAGAWIWA MBEGU

Na RENATHA KIPAKA-KARAGWE

WILAYA za Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera, zimewagawia mbegu za malando kwa kwa ajili ya wakulima ili kuanzisha kilimo cha biashara cha viazi lishe kujipatia kipato na kuongeza mnyororo wa thamani wa kilimo hicho.

Hatua hiyo, imetokana na wakulima wa wilaya hizo kupewa mbegu za marando ya aina ya Kabodei na Simama kwa ajiri ya kuanzisha mashamba darasa na kuhifadhi mbengu ambazo zitauzwa ndani ya wilaya hizo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Utafiti Kanda ya Ziwa wa Jukwaa la Kilimo la None State Actors (ANSAF), Audax Lukonge, alisema wameanza kutoa  elimu ya kilimo cha biashara na uongezaji wa mnyororo wa thamani kwa zao hilo.

Alisema wameamua kutoa mbegu hizo kuwasaidia wakulima kujipatia kipato na kuongeza myororo wa thamani wa zao hilo  kupitia  uzalishaji mbegu zitakazo uzwa kutoka kwenye mashamba darasa ya mradi huo.

“Mbegu hizi zitawapa faida wakulima kwanza zinatoa mavuno mengi na pili yanasoko, hivyo niwaombe kuzitumia kwa kuzingatia maelekezo ya maofisa ugani itakuwa na mafanikio zaidi.

“Makundi ya pamoja kwa ushirikano wa kilimo ni njia nyingine ya kuwapata wateja ambao hutafuta bidhaa kwa magari makubwa ambayo yanakwenda nje ya mikoa,”alisema Lukonge.

Naye Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Karagwe, Adamu Salumu alisema  fursa hii ya kupewa mradi wa shamba darasa itasaidia zaidi wananchi kuacha kutumia aina moja ya chakula ambacho wengi hula kwa mazoea.

Alisema licha ya chakula pekee ongezeko la kipato cha mafanikio na kupata uchumi kwa faida zinazoonekana baada ya mavuno na kuzalisha bidhaa  kwenye zao la viazi lishe.

Alisema Wilaya ya Karagwe, inakata kata 23 zilizoko kwenye mradi huo ulioanza Mei, mwaka huu katika kijiji cha Bujuruga.

 

Kwa upande wake, mkulima na mwezeshaji wa shamba hilo, Charles Wilbard alisema,mradi huu umefika kwa muda mwafaka kwani wakulima waliowengi walikuwa wakilima mazao ya aina moja pekee ya kibiashara.

 

Wilbard alisema, kilimo hicho kitapanua fikra za wengi kwa kulima na kuvuna mazao ya muda mfupi kisha kupeleka sokoni kutafuta riziki tofauti na mazao ya muda mrefu ambayo hutumia misimu mirefu kufikia hatua ya kuvuna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles