30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

UTORO WAWATIMUA KAZINI WALIMU 15 MSALALA

NA PASCHAL MALULU-KAHAMA

WALIMU 15 wa Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga,wamefukuzwa kazi kwa kosa la utoro kazini.

Watumishi hao,wamefukuzwa na Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo.

Akitoa taarifa ya kufukuzwa walimu hao, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege, alisema baada ya Kamati ya Maadili  kuwakuta na makosa, walimu 10 ilikubaliana kwa pamoja kuwafukuza kazi.

Alisema walimu wengine wanne wanapaswa kurudisha mishahara waliokwisha muda ambao hawakuwa kazini, huku mwalimu mmoja faili lake likihamishiwa Halmashauri ya Mji wa Kahama,baada ya kubainika kuwa siyo mwajiriwa tena.

“Walimu 10 wamefutwa kazi, walimu wanne wameamuliwa kufutwa kazi pamoja na kurudisha fedha ya mishahara ambayo walikuwa wanalipwa,bila kufanya kazi na mwalimu mmoja ameachiwa huru ambaye faili lake limepelekwa kwa mwajiri wake ambaye ni halmashauri ya mji wa Kahama kwani alikuwa yupo katika halmashauri yetu kumbe mwajiri wake ni mwingine,” alisema Berege.

 

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mibako Mabubu, alisema halmashauri hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali za nidhamu watumishi wanaofanya kazi kinyume na maadili ya ajira zao, huku akimuomba Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri kuendelea kuwafuatilia watumishi ambao hawaendani na maadili ya kazi zao hususani maeneo ya vijijini.

“Sisi kama baraza la madiwani tukuombe mkurugenzi kupitia idara yako ya utumishi iendelee kutuletea watumishi ambao wamejigeuza miungu watu hasa vijijini wanafanya kazi wanavyotaka sasa hawa hawatufai bora waondolewe wakafanye kazi wanazoona wao zinawafaa,” alisema Mabubu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles