23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAWEKEZAJI WAPEWA MAELEKEZO

Na BENJAMIN MASESE-MISUNGWI

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Amour Hamad Amour, amesema uwapo wa shule binafsi ni muhimu  na kuzitaka  kuwafundisha wanafunzi historia ya Tanzania, ilipotoka  na waasisi wake, badala ya kujikita kujua kuzungumza lugha ya kiingereza.

Kauli hiyo, aliitoa juzi wakati akifungua shule  binafsi ya Msingi ya Rishor iliyopo Wilaya ya Misungwi yenye wanafunzi  254 kuanzia  chekechea  hadi darasa sita.

Alisema mtoto mdogo, anatakiwa kujengewa misingi imara ya  elimu  bora sambamba na kufundishwa historia au chimbuko la Tanzania na waasisi wake, ambapo itaiwasaidia kujua jinsi gani  mababu wao walivyopambana hadi kupata uhuru bila  kumwaga damu.

“Shule za  english medium ni muhimu, ni chachu katika sekta ya elimu isitoshe Watanzania wengi wanaziamini  zinatoa elimu bora, nisema jambo  moja naombeni shule hizi pamoja na mipango yao zikumbuke kufundisha historia ya Tanzania na waasisi wake.

Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Rishor,Baraza Jackson alisema shule hiyo ilianzishwa kwa lengo la kkukuza sekta ya elimu, kutoa ajira na kuondoa adha ya wakazi wa maeneo la Idetemya kutembea umbali mrefu wa kupeleka watoto shuleni.

Alisema  mpaka hapo shule ilipozinduliwa ikiwa na wanafunzi wa chekechea hadi darasa la sita imegharimu Sh milioni 670, ikiwa ni ujenzi wa majengo, ununuzi wa ardhi ajira kwa wafanyakazi wapatao 40 ambapo alisisitiza upanuzi  wa miundombinu unaendelea kadri mahitaji husika yanavyojitokeza.

Wakati huo huo, Amour aliuomba uongozi wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Mwanza Gas Ltd,  kuwa mfano wa uwekezaji wenye tija wa kulipa kodi na kuzingatia sheria za nchi.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi, alisema uwekezaji huo ni mzuri na kuwataka kutoa ajira kwa watanzania hususan wa Misungwi.

Kwa upande wa upande wa Mkurugenzi wa Mwanza Gas Ltd, Habibu Nyakongeza, alisema  lengo la kuanzisha kiwanda hicho kwa ajili ya matumizi ya nishati ya gesi ya nyumbani huku walengwa wakuu ni wakazi wa Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles