Na MASYENENE DAMIAN,
WATAALAMU wa macho katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza wameishauri wawezeshwa kupata miundombinu ya tiba ya kisukari cha macho hospitalini hapo.
Daktari Bingwa wa Macho kutoka Bugando, Dk. Christopher Mwanansao amesema wagonjwa wengi wamekuwa wakihangaika kupata tiba yake.
Alisema wagonjwa wa kisukari cha macho wanaogundulika hospitalini hapo huangaika kupata matibabu kwa vile matibabu yake kutolewa na Hospitali za CCBRT, Dar es Salaam na KCMC, Moshi hapa nchini.
“Wagonjwa wanaokuja hapa katika kliniki yetu wanakuwa wamefikia stage (hatua) mbaya inayohitaji tiba ya mionzi ambayo sisi hapa hatuna hivyo hulazimika kuwepeleka KCMC.
“Hapa kwetu tunapima na kugundua tatizo na kutoa tiba kwa wagonjwa ambao bado hawana matatizo makubwa kwa kuwapa tiba ya sindano.
“Hiyo ni kwa ajili ya kuzuia utengenezaji wa mishipa ya bandia inayoweza kuharibu ubongo na figo, hivyo tunahitaji serikali iwekeze katika tiba hii kwa sababu wagonjwa wanaongezeka na tatizo linazidi kuwa kubwa,” alisema.
Mkuu wa Idara ya Macho katika hospitali hiyo, Dk. Evarista Mgaya alisema kwa wiki wanapata wagonjwa watatu hadi wanne wenye uhitaji wa tiba ya mionzi.
“Unajua takwimu za ugomjwa huu bado hazijawa sawasawa kwa sababu wagonjwa wanaofika hapa wengi ni wale wanaokuwa katika stage (hatua) mbaya.
“Wengi wanaishia katika hospitali za kawaida ambazo hazina uwezo wa kugundua tatizo hili na tuko kwenye mchakato wa kupata wafadhili wa kutupatia mionzi tuweze kutoa huduma hapahapa.
“Kanda ya Ziwa hakuna hospitali yenye huduma ya mionzi ya kutibu kisukari cha macho hivyo tunalilia kupata vifaa hivyo tuweze kutoa tiba hiyo hapa kwa sababu tunaweza kupima na kugundua tatizo la kisukari cha macho,” alisema na kuongeza: