24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WASHAURI WAWEZESHWE TIBA KISUKARI CHA MACHO

Na MASYENENE DAMIAN,

WATAALAMU  wa macho katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando   Mwanza wameishauri wawezeshwa  kupata miundombinu ya tiba ya kisukari cha macho hospitalini hapo.

Daktari Bingwa wa Macho kutoka Bugando, Dk. Christopher Mwanansao amesema wagonjwa wengi wamekuwa wakihangaika kupata tiba yake.

Alisema wagonjwa wa kisukari cha macho wanaogundulika hospitalini hapo huangaika kupata matibabu  kwa vile  matibabu yake kutolewa na Hospitali za CCBRT, Dar es Salaam  na KCMC, Moshi   hapa nchini.

“Wagonjwa wanaokuja hapa katika kliniki yetu wanakuwa wamefikia stage (hatua) mbaya inayohitaji tiba ya mionzi ambayo sisi hapa hatuna hivyo hulazimika kuwepeleka KCMC.

“Hapa kwetu tunapima na kugundua tatizo na kutoa tiba kwa wagonjwa ambao bado hawana matatizo makubwa kwa kuwapa tiba ya sindano.

“Hiyo ni kwa ajili ya kuzuia utengenezaji wa mishipa ya bandia inayoweza kuharibu ubongo na figo, hivyo tunahitaji serikali iwekeze katika tiba hii kwa sababu wagonjwa wanaongezeka na tatizo linazidi kuwa kubwa,” alisema.

 Mkuu wa Idara ya Macho katika hospitali hiyo, Dk. Evarista Mgaya alisema kwa wiki wanapata wagonjwa watatu hadi  wanne wenye uhitaji wa tiba ya mionzi.

 “Unajua takwimu za ugomjwa huu bado hazijawa sawasawa kwa sababu wagonjwa wanaofika hapa wengi ni wale wanaokuwa katika stage (hatua) mbaya.

“Wengi wanaishia katika hospitali za kawaida ambazo hazina uwezo wa kugundua tatizo hili na tuko kwenye mchakato wa kupata wafadhili wa kutupatia mionzi   tuweze kutoa huduma hapahapa.

“Kanda ya Ziwa hakuna hospitali yenye huduma ya mionzi ya kutibu kisukari cha macho hivyo tunalilia kupata vifaa hivyo  tuweze kutoa tiba hiyo hapa kwa sababu tunaweza kupima na kugundua tatizo la kisukari cha macho,” alisema na kuongeza:

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles