26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

RC ATAHADHARISHA MAFUA MAKALI YA NDEGE

Na Renatha Kipaka,

MKUU wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu ametahadharisha kuhusu mafua makali ya ndege ambayo yapo katika nchi jirani ya Uganda.

Amesema  kila mwananchi anatakiwa kuchukua hatua za tahadhari   ili ugonjwa huo usiingie nchini kupitia Mkoa wa Kagera.

Jenerali Kijuu alisema hiyo ni kwa kuzingatia mkoa huo unapakana na   Uganda na pia unazungukwa na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema  wananchi wa Kagera wanao wajibu mkubwa wa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa mafua makali ya ndege  Uganda zilithibitishwa na waziri mwenye dhamana na maenedeleo ya mifugo nchini humo Januari  15 mwaka huu.

Alitaja maeneo yaliyoathirika kuwa ni yale yanayozunguka ziwa Victoria na maeneo ya ndani ya ziwa katika wilaya za Entebbe na Masaka.

Taarifa za awali zilieeleza kutokea vifo vingi vya ndege pori katika Ghuba ya Lutembe kandokando ya ziwa Victoria karibu na mji wa Entebbe.

Taarifa hizo  zilitolewa na wavuvi wa sehemu hiyo.

Kwa mujibu wa habari hizo, vifo hivyo vya ndege pori vilianza kuonekana Januari 2 mwaka huu kabla ya kupatikana taarifa  za vifo vya baadhi ya ndege wanaofugwa kama kuku na bata katika Wilaya ya Masaka.

Januari 18 mwaka huu Waziri wa Afya, Maenedeleo ya Jamii,

Jinsi, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alitoa taarifa  kuhusu kuwapo  virusi vya ugonjwa huo nchini ya Uganda.

 Jenerali Kijuu alisema ugonjwa huo unaenezwa kwa kugusana na ndege wanaofugwa au wa pori, majimaji au damu ya ndege wenye virusi vya ugonjwa wa mafua makali.

“Pia unaenea kwa   kugusana na nguo zilizovaliwa wakati wa kuwahudumia kuku, matenga au magari yaliyotumika kusafirisha kuku na vifaa vilivyotumika kulishia kuku waliougua mafua ya ndege,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles