26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

KUTANA NA WANAWAKE WAREFU ZAIDI DUNIANI

warefuUREFU mzuri huhesabiwa kama zawadi na umbo linalomwongezea mtu uzuri. Hata hivyo, kwa watu wengine unaweza kuleta changamoto na matatizo hasa linapokuja suala la nguo, viatu, masuala ya kiafya na mengine ambayo wanaweza wasifurahie kutokana na urefu wao huo.

Kuna watu ambao hufa kutokana na urefu ‘good height’ wakati wengine wakifurahia na urefu mdogo lakini wenye kuvutia. Kwa watu wanaopenda michezo na uanamitindo urefu ni dhahabu. Wafuatao ni wanawake 10 warefu zaidi duniani.

Namba 10; Rita Miniva Besa

Mwanamke huyu kutoka Zimbabwe ambaye anaishi Marekani anashika nafasi ya tisa duniani akiwa na urefu wa futi sita na inchi 8.

Ni mchezaji wa mpira wa kikapu nchini humo kutokana na urefu alio nao. Ni mchezaji mkubwa wa mpira wa kikapu, maarufu na mwenye kipaji, ambacho msichana yoyote angependa kuwa nacho.

Namba tisa: Elisany da Cruz Silva

Msichana mwanamitindo wa  Brazil mwenye urefu wa futi sita na inchi tisa na ambaye ana rafiki wa kiume mwenye urefu wa futi tano na inchi nne. Binti huyo mwenye umri wa miaka 20 ni kivutio kikubwa nchini Brazil kutokana na urefu wake pamoja na umbo lake la kimodo.

 

Namba nane: Caroline Welz

Akiwa na urefu wa futi sita na inchi tisa, mwanamke huyu wa Ujerumani ni maarufu nchini humo na urefu wake ni kichocheo kwa watu wengi nchini humo. Ni msichana mrefu kuliko wengi wa umri wake duniani. Kuna watu wengi warefu Ujerumani, lakini Caroline ni tofauti, ndiye mrefu zaidi.

 

 Namba 7: Malee Duangdee

Mwanamke mrefu nchini Thailand, Malee Duangdee, anashika nafasi ya pili kwa urefu barani Asia akiwa na urefu wa futi sita na inchi 10.

Urefu wake uliotokana na matatizo ya uvimbe unaoharakisha ukuaji wa homoni ambazo zinamfanya kuwa mmoja wa wanawake wenye ukubwa duniani kwa nafasi ya saba.

Ana uzito wa kilo 127, njia pekee kwake kuishi maisha ya kawaida ni kupunguza uvimbe kwa kunywa dawa ambazo ni ghali mno kwa familia yao kuimudu.

Namba sita: Gitika Srivastava

Mwanamke huyo mwenye kipaji cha mpira wa kikapu mwenye urefu wa futi sita na inchi 11 ni mkazi wa India. Anashika namba sita kwa urefu duniani, ni kichocheo kwani anavutia watu wengi nchini humo. Baba yake pia alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu na alikuwa na urefu wa futi saba na inchi nne.

 

Namba tano: Uljana Semjonova

Mwanamke huyu kutoka Latvia anashika nafasi ya tano kwa wanawake warefu duniani na alicheza mpira wa kikapu katika miaka ya 1970-80 akiwa na urefu wa futi saba. Pia alikuwa akijulikana kama mchezaji wa mpira wa kikapu mwenye miguu mikubwa zaidi duniani. Huvaa viatu vya kiume vyenye saizi ya 21 kwa Marekani au 58 kwa Umoja wa Ulaya. Uijana ameshinda ubingwa mara 15 katika uliokuwa Muungano wa Kisovieti wa Urusi (USSR) na mara nyingine 15 Ubingwa wa Ulaya. Alikuwa mchezaji mzuri aliyeweka rekodi katika ngazi ya kimataifa pia.

 

Namba nne: Zainab Bibi

Mwanamke anayeshika nafasi ya nne kwa urefu ni Zainab Bibi kutoka Pakistan ambaye alihamia Uingereza baada ya familia yake kufedheheka kwa urefu wake huo. Ana urefu wa futi saba na inchi mbili.

Aliomba sehemu ya kuishi lakini ombi lake la ukimbizi lilikataliwa mwaka 2009 na hivyo kupewa kibali cha kuishi bure kwa miaka miwili mjini Manchester.

Namba tatu: Malgorzata Dydek

Akiwa amezaliwa Marekani na mchezaji wa mpira wa kikapu kutokana na urefu wake. Malgorzata Dydek, ana urefu wa futi saba na inchi mbili. Akiwa amezaliwa Aprili 1974 aliichezea Connection Sun katika ligi ya WNBA na aliikochi Northside Wizards. Aliwahi kuichezea Colorado Xplosion nchini Poland. Ameolewa na David Twigg, rafiki wake wa siku nyingi wa kiume huko Gdynia nchini Poland. Walihamia Brisbane, Australia baada ya ndoa yao na wamebarikiwa watoto wawili David na Alexander.

Namba mbili: Sandy Allen

Sandy Allen ni mwanamke mrefu namba mbili duniani. Awali alikuwa mrefu kuliko wote hadi 1976 na amefariki dunia mwaka 2008. Kwa mujibu wa Kitabu cha Rekodi za Dunia (GWR) alikuwa na urefu wa futi saba na inchi 7.5.

Urefu wake umetokana na kukua kwa homoni zake zilizotokana na uvimbe katika tezi pituitary, yaani tezi ubongo. Na alifanyiwa upasuaji bila mafanikio na kulazimika kutumia kiti cha magurudumu kumsaidia.

Kwa urefu wake huo alikabiliwa na matatizo mengi ya kiafya yaliyomfanya atumie sehemu kubwa ya miaka yake ya mwisho hapa duniani kitandani huko Indiana, Marekani.

Namba moja: Yao Defen

Yao Defen ndiye kinara wa wanawake warefu duniani akiwa amezaliwa China. Urefu wake wa futi saba na inchi nane ulitokana na matatizo ya kiafya na ana uzito wa kilo 200 na miguu mikubwa ya saizi 26 kwa vipimo vya Uingereza, 78 kwa Ulaya. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 40 Novemba 13, 2012. Yao alizaliwa katika familia masikini ya wakulima huko Liuan, Shucheng.

Kutokana na umasikini familia yake haikuwa na uwezo wa kugharimia matibabu yake. Na kutokana na udhaifu wa kiafya ilimwia vigumu kuwa nyota wa michezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles