30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Sababu za wanafunzi kupenda kusoma majuu

Chuo Kikuu cha Saint Marys cha Canada
Chuo Kikuu cha Saint Marys cha Canada

NA FARAJA MASINDE,

KILA mwaka idadi ya wanafunzi wanaokwenda kuchukua taaluma zao katika vyuo mbalimbali vya kimataifa imekuwa ikiongezeka.

Ziko sababu mbalimbali ambazo zinawafanya wanafunzi wengi kwenda kusoma kwenye vyuo vikuu vya kimataifa na kuacha vyuo vyao vya ndani.

Swali hilo la kwanini usome nje limekuwa likichukua nafasi kubwa zaidi na hii inatokana na kongezeka kwa mawakala wa vyuo vya kimataifa kila kukicha.

Wanafunzi wengi wanaona ni bora kupata taaluma zao za juu kama shahada ya udhamivu na nyingine kwenye vyuo vya kimataifa kuliko vile vya ndani.

Hata hivyo licha ya kuwapo kwa sababu mbalimbali lakini hizi ni baadhi ya zile ambazo zinaelezwa kuwa muhimu zaidi katika kuwasukuma wanafunzi kwenda kusoma nje ya nchi.

Uzoefu wa chuo kwenye taaluma husika

Uzoefu wa kimataifa unaotolewa kwenye taaluma husika ili uhakikisha kwamba inakuwa rahisi kupata soko kutokana na vyuo vinavyotambulika na uzoefu wa kimataifa.

Vyuo vya mataifa kama Uingereza, Marekani, Ujerumani, Australia na Canada ni kati ya vile ambavyo vimekuwa mstari wa mbele kutokana na uzoefu mkubwa wa taaluma mbalimbali zinazotolewa na vyuo vyake na hivyo kufanya viheshimike duniani kote.

Kwa wanafunzi wengi wa kimataifa eneo la uzoefu wa chuo ni jambo la muhimu kwa sababu inakuwa ni rahisi kupata ajira kokote duniani.

Kujifunza maisha na tamaduni tofauti

Kwa kiwango kikubwa wanafunzi wengi wamekuwa wakitumia fursa ya kwenda kusoma nje ya nchi na kutumia miaka mingi nchini humo hali inayowasaidia kujifunza tamaduni mpya kutoka kwenye mataifa hayo.

Sababu hiyo inaelezwa kwamba imekuwa ikiwasaidia wengi katika kuwajengea stadi za maisha na hata kuweza kumudu kuishi maisha ya ng’ambo na hata kutafuta kazi kwenye mataifa husika pindi wanapohitimu masomo yao.

Aambapo wanakuwa tayari na mbinu juu ya namna ya kukabiliana na waajiri wa mataifa hayo na hata wale wa kimataifa.

Ufadhili na ada nafuu

Sababu hii pia inachukuliwa kama moja ya zile zinazochangia kwa wanafunzi wengi kupenda kusoma nje ya nchi, kwani asilimia kubwa ya wanafunzi wa mataifa ya kigeni wanaosoma kwenye vyuo vya kimataifa wamekuwa wakipata ufadhili pamoja na unafuu wa ada na hivyo kujikuta kila mtu akihitaji kutumia fursa hiyo.

Inafahamika wazi kuwa ni gharama kubwa kusoma kwenye vyuo hivyo vya kimataifa hivyo ndio maana wengi wamekuwa wakitumia fursa hiyo ya ufadhili kwenda kusoma nje kuliko kwenye mataifa yao.

Hata hivyo nafuu huo unategemeana na aina ya masomo anayosoma mwanafunzi husika, gharama bila kusahau zile za makazi.

Lakini kuna unafuu mkubwa wa kusoma kwenye mataifa hayo yaliyoendelea mfano kama unaishi nchini, Marekani na ukahitaji kusoma nchini Ujerumani basi utakuwa umeokoa kiasi kikubwa cha fedha kutokana na ufadhili unaotolewa na baadhi ya vyuo nchini humo.

Kuimarisha ujuzi wa lugha

Idadi kubwa ya wanafunzi wanapenda kujifunza changamoto mpya kutoka kwenye mataifa yanayotumia lugha tofauti ili kuimarisha uwezo wao wa kuzungumza lugha.

Hivyo wengi wamekuwa wakipendelea kusoma kwenye mataifa hayo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanakuwa na uwezo mkubwa wa lugha za kigeni ili kukabili ushindani wa ajira uliopo kwasasa.

Kwenye vyuo vingi inapofikia mwanafunzi anachukua elimu ya juu basi wamekuwa wakitoa masomo ya lugha mbalimbali bure kulingana na nchi aliyopo na hivyo kumsaidia kujiongezea ujuzi wa lugha.

Kujenga mahusiano na wakufunzi wa kimataifa

Hii nayo ni moja ya siri kubwa ambayo imekuwa ikiwasukuma  wanafunzi wengi kwenda kusoma kwenye mataifa mbalimbali yaliyoendelea, wengi wamekuwa wakihitaji kujenga mahusiano bora na wakufunzi wa vyuo vya kimataifa ili iwe rahisi kuwaunganisha kwenye makampuni mbalimbali duniani kutokana na uzoefu wao.

Hizo ni baadhi tu ya sababu zinazowasukuma wanafunzi wengi kwenda kusoma masomo katika vyuo vya kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles