26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hollande aichokonoa Uingereza

Francois Hollande
Francois Hollande

PARIS, Ufaransa

RAIS  Francois Hollande wa Ufaransa, ameichokonoa Serikali ya Uingereza kwa kumhimiza waziri mkuu wa nchi hiyo, Theresa May, aharakishe mazungumzo ya nchi yake kutoka Umoja wa Ulaya (EU).

Kwa mujibu wa DW, Rais Hollande, amesisitiza umuhimu wa Uingereza kuharakisha talaka yake ya kujitoa EU, ingawa amekiri wazi kwamba May anahitaji muda wa kutosha kuratibu talaka hiyo.

“Bora ikiwa haraka kwa masilahi ya pande zote, Umoja wa Ulaya, Uingereza na kwa shughuli za kiuchumi za pande zote mbili,” alisema Hollande.

Kauli hiyo ya Hollande ambayo aliitoa jana, imekuja siku moja  baada ya Kansela wa Ujerumani,  Angela Merkel, kuunga mkono wito wa Waziri Mkuu Mpya wa Uingereza,  Theresa May wa kupatiwa muda wa kuandaa mazungumzo rasmi yatakayoitoa Uingereza ndani ya EU.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa Uingereza, alijibu mapigo kwa kuahidi kutilia mkazo umuhimu wa kuendelezwa mazungumzo ya nchi yake kujitoa EU katika njia ya utulivu.

May alisema kuwa atahakikisha haki za raia wa nchi za Umoja wa Ulaya wanaoishi Uingereza zinaheshimiwa Uingereza itakapotoka katika Umoja huo.

“Kwa kuwazingatia Wafaransa wanaoishi Uingereza wakati tukiwa wanachama kamili wa Umoja wa Ulaya, bila ya shaka hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwa Waingereza wanaoishi Ufaransa au katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

“Siku zijazo nataka kuwa na uwezo wa kudhamini haki za wakazi wa EU na ningependelea kuwa na uwezo wa kufanya hivyo, njia pekee itakayopelekea hayo yasiwezekane ni kama haki za raia wa Uingereza wanaoishi katika mataifa ya EU,” alisema May.

Uingereza pekee ndiyo itakayoamua lini kukitumia kifungu nambari 50 cha makubaliano ya Umoja wa Ulaya kuhusu kujitoa katika umoja huo.

Maombi rasmi yatakapotolewa, majadiliano yataanza na kumalizika miaka miwili inayokuja, ikimaanisha Uingereza itatoka rasmi mwaka 2019.

Akiwa mjini Berlin, Jumatano iliyopita, May alisema nchi yake haitatuma maombi rasmi ya kujitoa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles