22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Meya amwomba radhi Keita wa Lazio

Keita Balde
Keita Balde

LAZIO, ITALIA

MEYA wa mji wa Padova nchini Italia Massimo Bitonc, amemwomba radhi mshambuliaji wa Lazio, Keita Balde kutokana na kitendo cha kibaguzi kilichofanyika wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Padova inayocheza Ligi Daraja la Tatu nchini humo (Lega Pro).

Kitendo hicho kilitokana na mashabiki wa timu hiyo  kushangilia mithili ya nyani mbele ya mshambuliji huyo wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi.

Keita, ambaye alizaliwa nchini Hispania na wazazi wenye asili ya  Senegal, alianza kukipiga katika kikosi cha  Barcelona kabla ya kuhamia  Italia mwaka 2011.

Nyota huyo alikuwa sehemu ya wachezaji wa Simone Inzaghi waliocheza dhidi timu ya daraja la tatu.

Lakini katika tukio linalofanana na hilo mwaka 2013, Kevin Prince Boateng alifanikiwa kuwaongoza wachezaji wenzake nje ya uwanja.

Keita alionekana kuwa pekee katika kitendo hicho cha unyanyasaji na ubaguzi.

Keita (21) licha ya kufanyiwa kitendo hicho aliendelea kubaki uwanjani kusaidia timu yake kushinda mabao 2-1.

Hata hivyo baadae Meya wa jiji hilo Bitonc, alisema kwamba; “Michezo ni raha na inahitaji ushirikisho na urafiki.

Naomba radhi kwa kusikia kilichotokea, kama Meya na mwanamichezo, kilichotokea usiku wa jana (juzi) kiliudhi kila mtu wa jiji hili hususani ni mashabiki wa ukweli wa soka wanaotumia uwanja huu.”

Meya huyo alimalizia kwa kuomba msamaha kwa Keita kwa niaba ya mashabiki na wapenda michezo wa jiji hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles