31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Namba ya Pobga ipo wazi Manchester

pogba

MANCHESTER, ENGLAND

MGAO wa namba za jezi  tayari umepita katika klabu ya Manchester United huku ikibaki jezi namba 6 ambayo imedaiwa huenda ikawa kwa ajili ya ujio wa kiungo wa Juventus, anayetaka kusajiliwa na klabu hiyo, Paul Pogba.

Katika mgao huo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Zlatan Ibrahimovic amekabidhiwa jezi namba 9 iliyokuwa ikivaliwa na nyota mwingine wa timu hiyo, Anthony Martial ambaye kwa sasa atavaa namba 11.

Nyota huyo wa Sweden, alikuwa na machaguo matatu ya namba kati ya namba 8, 9 na 10  tangu atue Old Trafford na alitarajiwa kuchagua namba tofauti na hizo ingawa ilikuwa tofauti.

Lakini Martial ametupwa hadi namba 11 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Adnan Januzaj ambaye sasa anavaa namba 15.

Juan Mata amefanikiwa kubakia na  namba 8 na Wayne Rooney kubaki na namba 10.

Mchezaji mwingine mpya wa timu hiyo, Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan wamepewa namba tatu na 22.

Hata hivyo baada ya mgawo huo imesalia namba 6 ambayo inadaiwa huenda imetunzwa kwa ajili ya ujio wa Paul Pogba ambaye anavaa namba inayofanana akiwa Juventus.

Mashabiki wa timu hiyo wana hamu ya kumuona Ibrahimovic akivaa namba 9 wakati itakapokuwa kwenye safari ya michezo wa maandalizi ya msimu mpya nchini China.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles