33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Huyu ndiye Mbrazil anayedai ni Yesu

3

Na JOSEPH HIZA,

MIAKA 2000 iliyopita, wakati alipoulizwa na wanafunzi wake kuhusu ishara ya mwisho wa dunia na ya kurudi kwake duniani, Yesu Kristo aliwajibu;

“Na mtasikia vita na minong’ono ya vita na taifa litainuka dhidi ya taifa, falme dhidi ya falme na kutakuwa na baa la njaa, magonjwa ya kuambukiza na matetemeko makubwa ya dunia sehemu mbalimbali na kutakuwa na kila aina ya uasi.

Aidha, Yesu alitahadharisha katika siku hizo za mwisho kutakuwa na utitiri wa manabii wa uongo.

Zama hizi tunashuhudia kutumia kwa utabiri huo katika dunia hii iliyotawaliwa na migogoro ya kidini, kisiasa, kijamii, kutokuwapo usawa.

Aidha, inashuhudia kubadilishwa kwa asili ya maumbile ya mwanadamu pamoja na ongezeko la majanga ya asili yanayochagizwa zaidi na mwanadamu mwenyewe, rejea mawakala wa mabadiliko ya tabia nchi.

Licha ya hayo kuna manabii wengi wa uongo wanaoliimba jina lake.

Nchini Brazil, kuna mwanamume anayedai kuwa ni Yesu aliyerudi duniani katika mwili mwingine, ambaye wafuasi wake wanamuamini ndiye, lakini pia wengi wakimweka kundi moja na manabii wale wa uongo.

Septemba 1979, wakati wa kipindi cha mfungo huko Santiago nchini Chile, Inri Cristo anadai kupata maono kuhusu utambulisho wake kuwa yu Kristo katika mwili mwingine ambaye alifufuka miaka 2,000 iliyopita.

Katika safari yake ndefu duniani, Inri amehojiwa na mamia ya waandishi wa habari katika miji mikuu yote ya Amerika ya Kusini na Ulaya pamoja na miji mikubwa ya Brazil.

Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 68 ameitumia miaka 35 akihutubia neno la Mungu kwa sababu anaamini yeye ni Yesu katika mwili mpya.

Inri Cristo ana mamia ya wafuasi duniani ikiwamo nchini Uingereza, Ufaransa na Brazil ambao baadhi wanaishi naye katika kanisa lake lililopo kwenye kiwanja kimoja mjini Brasilia.

Tangu 1979 ametembelea nchi 27 akisambaza neno lake, lakini mitazamo yake yenye utata imeshuhudiwa akitimuliwa nchini Marekani, Uingereza na Venezuela.

Wengi wa wanafunzi wake ambao wanaishi katika kanisa lake, sehemu kubwa wakiwa wanawake wamemfuata Inri kwa miongo kadhaa, mzee kuliko wote akiwa Abevere, (86) ambaye amefuatana naye kwa miaka 32.

Mwanafunzi wake mdogo kuliko wote kwa sasa ana umri wa miaka 24 na alikutana naye mara ya kwanza na Inri wakati akiwa na miaka miwili tu.

Kama Yesu aliyezaliwa upya’ amechukua jina la Inri, ambalo ni ufupisho wa kilatini uliokuwa umeandikwa msalabani wakati wa kusulubiwa kwa Yesu na unasimama kwa Jesus Nazarenus, Rex Iudaeorum, au : Yesu Mnazareti, Mfalme wa Wayahudi’ na Cristo, linamaanisha Kristo.

Wakati asipokuwa na kazi ya kuhubiri au kujumuika na wafuasi wake, Inri Cristo hupenda kuzunguka na skuta yake.
Wakati asipokuwa na kazi ya kuhubiri au kujumuika na wafuasi wake, Inri Cristo hupenda kuzunguka na skuta yake.

Uvaaji wake kama Yesu na msimamo wake mkali wa namna anavyochukulia ubepari, utoaji mimba na hata Krismasi umesababisha akamatwe na polisi mara 40.

Anasema: “Najua kuna watu wasio na idadi kote Brazil na duniani ambao mioyo yao ipo pamoja nami.”

Lakini pamoja na kujiona mwenyewe kuwa Yesu katika mwili mpya, Inri hukataa kusherehekea sikukuu ya Krismasi akisema ni siku ambayo ‘matajiri huwaumiza masikini’.

“Ni siku ambayo watoto wa matajiri wanaweza kuonesha zawadi wanazopokea huku watoto wa masikini wakibakia kuumia. Hivyo ni siku ya huzuni kwa yeyote anayeona vitu kwa macho kama nionavyo,” anasema.

Inri anasema mara ya kwanza alipokea ufunuo kwamba yeye ni Kristo wakati wa mfungo wa kidini mjini Santiago, Chile mwaka 1979.

Tangu utoto wake, anasema amekuwa akifuatilia sauti yenye nguvu ambayo huzungumza katika kichwa chake lakini ilikuwa wakati huo ilipomwambia: “Mimi ni Baba yako. Mungu wa Abraham, Isaac na Jacob.”

Kwa sasa anaendesha kanisa lake mwenyewe, the ‘Soust’ (Suprema Ordem Universal da Santmssima Trindade), lililopo eneo la mashambani nje kidogo ya Brasilia, mji mkuu wa  Brazil, ambalo huliita ‘Yerusalem Mpya’.

Yeye na wafuasi wake wamekuwa wakishindia matunda kama vile ndizi, parachichi na maembe pamoja na mboga za majani.

Pia kuna kanisa dogo ambako Ingra huzungumza na wafuasi wake kila Jumamosi asubuhi na nyumba kwa ajili ya mbwa ambao hulinda eneo hilo.

Maisha yake yasiyo ya kawaida yamewafanya wakosoaji wake kusema ana ugonjwa wa akili, tuhuma ambazo amekuwa akizikana vikali.

“Naweza kuwa na wazimu lakini si bubu. Wazimu ni tofauti na maradhi ya akili. Ni mama wa wanafarsafa, manabii na wavumbuzi.

‘Dhima yangu ni kujiandaa kuchagua manusura wa bomu la nyuklia ambalo litapelekea mwisho wa dunia hii ya fujo, kwa ajili ya uumbaji wa jamii mpya, ambayo iko kwa ajili ya kutimiza matakwa ya muumbaji,” anasema.

Pia aliwahi kutabiri mwisho wa dunia kuwa mwaka 2012. Wakati utabiri ulipofeli, alidai alimaanisha 2012 utakuwa mwisho wa dunia kwa wale tu ambao watafariki mwaka 2012.

Hata hivyo, Inri Cristo si mtu pekee kuwahi kudai kuwa yeye ni Yesu aliyerudi duniani. Miongoni mwao ni pamoja na John Miller.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles