26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Miss Kilimanjaro 2016/2017 kupatikana leo usiku

MISS Kilimanjaro 2016/2017
MISS Kilimanjaro

NA SAFINA SARWATT, KILIMANJARO

MISS Kilimanjaro 2016/2017 atakayewakilisha Mkoa wa Kilimanjaro katika mashindano ya urembo kitaifa mwaka huu anatarajia kupatikana leo usiku katika shindano litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Kill home uliopo Moshi mjini.

Mrembo atakayepatikana usiku wa leo atatoka kati ya warembo 22 wanaotarajiwa kushindana katika shindano hilo.

Mratibu wa Miss Kilimanjaro 2016/2017, Dotto Sang’wa, kupitia Kampuni ya Dee’s Bridal, alisema washiriki hao wanatoka wilaya saba za mkoa huo.

“Mwanzoni tulikuwa na jumla ya warembo 30, lakini watano tuliwaondoa kutokana na kukosa sifa za kushiriki mashindano hayo na wengine watatu ni wagonjwa hivyo hawataweza kushiriki,” alieleza Dotto.

Katika shindano hilo wasanii Navy Kenzo na Makomandoo watatumbuiza huku kiingilio cha juu kikiwa Sh 40,000 na chini ni Sh 20,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles