Juliana Samweli, TUDARCo
Mabasi ya abiria maarufu kwa jina la mwendokasi, yameanza safari za kupitia barabara Shekilango kuelekea Mwenge leo Alhamisi Agosti 26, ikiwa ni njia mpya tofauti na awali zilikuwa zikipita barabara ya Morogoro na Ali Hassan Mwinyi pekee.
Mabasi hayo yalioneka asubuhi ya leo yakiwa yabeba abiria wa kutoka Shekilango hadi Mwenye.
Mtanzania Digital ilishuhudia mabasi hayo katika barabara ya Shekilango, huku abiria wakionekana kufurahia huduma hiyo.
Awali mabasi hayo yalikuwa yakifanya safari zake, Mbezi, Kimara, Morocco, Kariakoo Gerezani, Kivukoni na Muhimbili.
Mmoja wa abiria amesema ujio wa mabasi hayo katika njia ya Shekilango, itasaidia kurahisisha usafiri na kupunguza msongamano kwenye daladala.