27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mabasi ya mwendokasi yaanza kupita njia mpya

Juliana Samweli, TUDARCo

Mabasi ya  abiria maarufu kwa jina la mwendokasi, yameanza safari  za kupitia  barabara  Shekilango kuelekea Mwenge leo Alhamisi Agosti 26,  ikiwa ni njia mpya tofauti na  awali zilikuwa zikipita  barabara ya Morogoro na Ali Hassan Mwinyi pekee.

Mabasi hayo yalioneka asubuhi ya leo yakiwa yabeba abiria wa kutoka Shekilango hadi Mwenye.

Mtanzania Digital ilishuhudia mabasi hayo  katika barabara ya Shekilango, huku abiria wakionekana kufurahia huduma hiyo.

Awali mabasi hayo yalikuwa yakifanya safari zake, Mbezi, Kimara, Morocco, Kariakoo Gerezani, Kivukoni na Muhimbili.

 Mmoja wa abiria amesema ujio wa mabasi hayo katika njia ya Shekilango, itasaidia kurahisisha usafiri na kupunguza msongamano  kwenye daladala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles