24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digitala

Serikali imesaini makubaliano na Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yenye lengo kusaidia sekta ya vyombo vya habari nchini.

Akizungumza Juni 3, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nauye amesema wamefanya mambo mengi na UNESCO katika sekta mbalimbali nchini.

“Makubaliano haya yamelenga kuhimarisha uchumi wa vyombo vya habari na kuona namna ya kusaidia uhuru wa vyombo vya habari, usalama na ulinzi kwa waandishi wa habari hasa wanapotimiza majukumu yao,”amesema Nape.

Ametaja jambo jingine kuwa nikutoa mafunzo ya kuendelea kwa waandishi habari kuhamasisha mazingira sera na sheria za vyombo vya habari na kuimarisha mfumo wa kidigital sambamba na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na UNESCO.

Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Michelle Toto amesema makubaliano hayo yamelenga vyombo vya habari ambayo ni muhimu na kusaidia tasnia hiyo.

“Makubaliano haya ni ya kwanza kusaini nchini Tanzania yatatoa fursa na maslahi kwa wadau wa vyombo vya habari na kujadili changamoto mbalimbali na kulinda haki za waandishi,”amesema Toto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles