24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto wa MNEC Jumaa waunga mkono juhudi za Rais Samia

*Watoa shuka 200 kituo cha afya Mlandizi

Na Gustafu Haule, Pwani

WATOTO wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(MNEC), Hamoud Jumaa, wametembelea kituo cha afya Mlandizi kilichopo Kibaha Vijijini mkoani Pwani na kutoa msaada wa shuka 200 zenye thamani ya Sh milioni 4 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kunyanyua sekta bya afya.

Watoto hao Mariam Jumaa na Hanifa Jumaa wametoa msaada huo Juni 4 kwa kushirikiana na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kibaha vijijini chini ya mwenyekiti wake Livinus Cleophace na Katibu wa Umoja huo Zainabu Mketo.

Wakikabidhi msaada huo kwa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk. Sebastian Misoji, wamesema wameamua kutoa msaada huo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia ambaye anafanyakazi kubwa ya kuwatumikia wananchi ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali kote nchini.

“Juhudi hizo zinapaswa kuungwa mkono na watu wote ndio maana sisi familia tumeamua kujitoa na kumsaidia rais katika kupambana na changamoto ya ukosefu wa shuka katika kituo cha afya Mlandizi.

“Rais Dk.Samia anafanyakazi kubwa na sote tumeshuhudia jinsi ambavyo amekuwa akitoa kipaumbele katika kuboresha huduma za afya hususan wodi za wazazi ndio maana nasisi leo tumeona tuje hapa kumsaidia rais wetu katika kuunga mkono juhudi zake,”amesema Mariam.

Naye, Hanifa Jumaa, amesema uamuzi wa kutoa msaada huo umetokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina yao na uongozi wa UVCCM Kibaha Vijijini na kwamba wataendelea kusaidiana na jamii siku zote bila kuchoka.

“Leo tumefika hapa kutoa huu msaada wa shuka 200 zenye thamani ya Sh 4,000,000 ili kusaidia jamii na wananchi wa Kibaha Vijijini hususan wagonjwa wanaokuja kutibiwa hapa nina imani hata zile zahanati za pembezoni zitawafikia,”amesema Hanifa.

Katibu wa UVCCM Kibaha Vijijini, Zainabu Mketo, amesema umoja wa vijana umekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi rais.

Amesema kufika katika kituo cha afya Mlandizi siyo mara ya kwanza kwani wamekuwa wakitembelea kituo hicho mara kwa mara kwa ajili ya kujionea changamoto zilizopo na kisha kuzifanyiakazi.

Aidha ameishukuru familia ya Jumaa kwa kutoa msaada huo kwani anaamini unakwenda kuwanufaisha Watanzania wengi wanaopata huduma katika kituo hicho huku akiwaomba waendelee kusaidia na maeneo mengine.

Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk. Sebastian Misoji, amewashukuru watoto hao nakusema kuwa msaada huo umepunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya ukosefu wa shuka katika kituo hicho.

Amesema ili madaktari na wauguzi waweze kufanyakazi zao vizuri wanahitaji uwepo wa vifaa vya kutosha lakini kwa kituo cha Mlandizi wanafarijika zaidi kwakuwa wanapata ushirikiano mkubwa kutoka CCM na jumuiya zake.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles