28.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 2, 2021

30 kortini kwa mauaji ya watoto

MWANDISH WETU-NJOMBE

JESHI la Polisi kupitia Kitengo Maalumu cha Kupambana na Uhalifu, limesema kuwa hadi sasa tayari wametia mbaroni watuhumiwa 30 wanaodaiwa kuhusika na mtandao wa mauaji ya watoto mkoani Njombe.

Akizungumza jana Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu, Naibu Kamishna Liberatus Sabas, alisema kuwa tangu alipopiga kamo mkoani Njombe kwa kushirikiana na jeshi hilo mkoani hapa, wamefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa 30.

Kutokana na hali hiyo alisema kwa sasa wanakamilisha uchunguzi wao na huenda leo watuhumiwa hao wakafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

“Tangu tulipoiga kambi Njombe kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoa, tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 30 ambao kwa namna moja ama nyingine wanadaiwa kuhusika na mtandao wa mauaji ya watoto.

“Baada ya hatua hii tunatarajiwa watuhumiwa hawa tutawafikisha mahakamani Jumatatu (leo) na kubwa tunawaomba Watanzania waendelee kutoa taafa za watu watu wanaohusika na mtandao huu ili tuweze kuukomesha kabisa,” alisema Naibu Kamishana Sabas

Alisema katika operesheni hiyo hawatomuonea mtu yoyote.

“Katika hili hatutamuonea mtu yoyote ila kama wewew unahusika na mauaji haya hata kama ukiwa mfanyabishara, kiongozi wa serikali, dini au hata mganga wa tiba za asili utambue kwamba sheria itachukua mkondo wake,” alisema Sabas

Mwili wa mtoto Meshack Myonga (4), ambaye alifariki dunia juzi unatarajiwa kuwasili leo kutoka mkoani Mbeya alipopelekwa kwa matibabu baada ya kunusurika kuawa na kutekwa kwa kukatwa koromeo wilayani Njombe .

Mtoto  huyo alifariki dunia juzi akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Meshack alitekwa Desemba 23, mwaka jana mtu asiyejulikana akiwa nyumbani kwao Mtaa wa Mji Mwema wilayani Njombe, kisha kupelekwa msituni na kukatwa  koromeo kabla ya kuokolewa na mwananchi mmoja.

Baada ya hatua hiyo ya kuokolewa kwa mtoto huyo alipelekwa Hospitali ya Mkoa ya Kibena na baadaye  kuhamishiwa hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu .

Akizungumza na mama mzazi wa mtoto huyo, Rabia Mlelwa alisema baada ya kufika hospitali madaktari walimchukua na kuingia ndani n baada ya muda aliitwa na kuambiwa mtoto amefariki dunia.

“Wakati ule wanaingia nae ndani hawakuniambia lolote kuhusu maendeleo yake ila waliniambia mwanangu amefariki, wamesema mtoto koromeo lake lilikuwa limekaa vibaya hivyo alikuwa mtu wa kufa wakati wowote,” alisema Rabia

Mama huyo wa mtoto Meshack, alisema baadaya kupewa taarifa za kifo cha mtoto wake alipatwa na bumbuwazi asijue la kufanya.

Alisema baada ya mtoto wake kufikishwa hospitali hao alitakiwa kurudi tena hospitali hapo juzi ili kujua maendeleo ya mwanaye, baada ya kukaa wiki mbili katika hospitali hiyo wakipatiwa matibabu.

“Hata hivyo sina la kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo, Mkuu wa Wilaya ya Njombe (Ruth Msafiri) alitoa gari lililotuleta Mbeya, lakini baada ya tukio hili ametaarifiwa, hivyo  ameamuru gari hilo lirudi tena kwa ajili ya kutuchukua hivyo muda huu (jana) tupo njiani kurudi kijijini Ngalangwa  kwa taratibu za mazishi. Hakika mtoto wake amedhulumiwa uhai wake Mungu anajua roho inaniuma sina la kusema kwa sasa,” alisema Rabia

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,646FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles