Ray C: Umezima ni maalumu kwa Valentine

0
1758

JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema wimbo wake mpya wa ‘Umezima’ ni zawadi maalumu kwa mashabiki wake katika msimu wa Valentine.

Akizungumza hivi karibuni jijini hapa, msanii huyo alisema ameamua kuwapa burudani ya Valentine mashabiki ambao kwa muda mrefu wamekuwa na shauku ya kusikia zaidi kazi zake.

“Huu ni mwendelezo wa ujio wangu kwenye tasnia hii tena, natambua mashabiki watakuwa na shauku ya kunisikia zaidi, lakini niwajulishe tu nitaendelea kutoa kazi juu ya kazi ili kuwapa burudani,” alisema Ray C.

Mwanadada huyo ambaye ameonekana kurudi vema kwenye tasnia ya muziki, alisema anafarijika kusikia na kuona mashabiki wakipokea kazi zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here