21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

Polisi wasio waamini kuchunguzwa

KHAMIS SHARIF-ZANZIBAR

SERIKALI imesema kuwa itaunda tume ya kuchunguza askari wasio waaminifu ambao wanadaiwa kujihusisha na kuomba na kupokea  rushwa kama njia ya kupitisha dawa za kulevya katika Visiwa vyua Unguja na Pemba.

Hayo yalisemwa juzi na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni,  alipozungumza na waandishi wa habari kutokana na kuwapo   ongezeko la uingizwaji   dawa za kulevya visiwani hapa.

Alisema serikali haijaridhishwa na kasi ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya inayochukuliwa na polisi   Zanzibar.

Alisema ongezeko la uingizaji wa dawa za kulevya linatokana na baadhi ya askari wasio waaminifu kupokea rushwa na kuridhia kuingizwa kwa dawa ya kulevya hali inayosababiusha  kuwapa mwanya wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuendelea kuingiza biashara hiyo.

Alisema tume hiyo itakapokuja itachukua vielelezo vilivyopo  kupata urahisi wa kuwatambua askari hao kwa lengo la kuwachukulia hatua za  sheria.

“Tunataka tupate mtandao wote wa askari wanaochukua rushwa, hatuwezi kumvumilia askari anayeruhusu kuingizwa dawa za kulevya visiwani mwetu,” alisema Masauni.

Alisema hatua ya kuchukizwa na watendaji wasio waaminifu kwa kuendelea kuruhusu kuingizwa dawa za kulevya hali inayosababisha  kuharibika   vijana wanaotumia dawa za kulevya na hivyo kupoteza mwelekeo wao wa maisha.

“Hili jambo linaniumiza rohoni kuona vijana wetu wanapoteza mwelekeo wao kwa kutumia dawa za kulevya,” alisema Masauni.

Alisisitiza kuwa jeshi hilo halitawavumilia askari ambao hawatekelezi  wajibu wao ipasavyo na kuipeleka Zanzibar kuwa chaka la kuingiza dawa za kulevya.

“Hatuwezi kuendelea kukaa na askari ambao hawafanyi wajibu wao tukastahamili tu.

“Hadi leo kisiwa chetu kinashindwa kudhibiti dawa za kulevya tunatumia mwamvuli wa kujificha kupambana na dawa za kulevya kwa kutumia wahalifu,” alisema.

Novemba mwaka jana, Naibu Waziri Masauni, alilitaka Jeshi la Polisi kuangalia namna ya kuwapa mbwa mafunzo maalumu kunusa na kugundua dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali ya bandari na viwanja vya ndege   Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles