25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu atoa msaada S/Msingi Mbweni


Na AVELINE KITOMARY DAR ES SALAAM 

JAMII imeshauriwa kushirikiana na serikali kuboresha huduma mbalimbali ili kuchangia kasi ya maendeleo na kuunga mkono juhudi katika kupambana na umasikini. 

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Askofu wa Kanisa la Waadventisti wasabato Jimbo Kuu la Kusini, Mark Malekana wakati wa akitoa msaada kwa Shule ya Msingi Mbweni, Wilayani Kinondoni ambapo alisema msaada huo wa kuboresha elimu una thamani ya Sh millioni 7.

“Tumeamua kutoa msaada huu ili angalau kutatua changamoto za ukosefu wa meza,viti na makabati katika shule hii kwani walimu walikuwa wakisahihisha madaftari na mitihani kwenye madawati na wanafunzi lakini sasa watafanyakazi vizuri “alisema Askofu Malekana.

Aliongeza “Tutaendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma zingine lakini nitoe wito kwa taasisi zingine kujitokeza kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za jamii.

Mratibu wa Elimu Kata ya Mbweni, Angelina Rweyemera alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza adha wanayoipata walimu kwani mpaka sasa shule hiyo ina upungufu wa meza na viti huku ikiwa na walimu 22.

“Msaada uliotolewa utasaidia sana walimu kuondokana na adha katika kazi zao hivyo tunaomba wadau wengine waendelee kujitokeza kushirikiana na serikali katika kuinua elimu,”alisema Rweyemera.

Mwalimu  Mkuu wa shule hiyo, Moses Amani alisema wanashukuru kanisa hilo kwa kukubali kutatua changamoto hiyo kwani walipotuma ombila la kununuliwa vifaa hivyo walijibu kwa haraka.

Mmoja wa walimu wa shule hiyo, Doto Sebastian alisema hatua hiyo inawasaidia kupata vitendea kazi kwani wamekuwa wakisahihisha madaftari ya wanafunzi kwenye magoti kutokana na ukosefu wa meza.

“Tumefurahi tumepata vitendea kazi kwani wakati mwingine tulipokuwa tunasahihisha madaftari ya wanafunzi tulitumia magoti badala ya meza kwa hiyo wametusaidia sana,”alisema Doto.

Masaada huo ni pamoja ni meza 10, viti 10 na kabati tano za kuhifadhia kitabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles