24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waitara awaonya wapinzani

SAMWEL MWANGA,MASWA.

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mwita Waitara amewaonya viongozi na wanachama wa Vyama vya upinzani, watakaokwamisha utendaji wa viongozi wa Serikali za mitaa kwani walisusia kwa hiari yao uchaguzi uliofanyika Novomba 24, mwaka huu.

Waitara alisema hayo jana wilayani Maswa mkoani Simiyu, wakati akizungumza na viongozi mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku moja wilayani humo.

Alisema uchaguzi wa Serikali za Mitaa, umekwisha,ni vizuri viongozi wote waliochaguliwa ambao wanatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM), wakajiamini kwa kufanya kazi kwa sababu waliapishwa kisheria.

“Uchaguzi umeshamalizika, ninyi ndiyo viongozi mliochaguliwa ama kupita bila kupingwa,nyote humu mnatokana na CCM, mjiamini mlishakula kiapo cha kutumikia nafasi zenu fanyeni kazi zenu kwa uhuru kwa kufuata sheria kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi,”alisema.

Alisema  licha ya kuwepo matamko mbalimbali kutoka kwa vyama vya upinzani kutowapa ushirikiano kwa kile walichodai hakuwakupata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi na kuwataka wayapuuze.

“Kuna chama kimoja cha upinzani hivi karibuni kimefanya uchaguzi wake na kutoa matamko mbalimbali ya kutowatambua viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, niwahakikishieni msitishwe ninyi pigeni kazi kwani mnalindwa na sheria zilizoko katika nchi hii,”

”Na kupitia mkutano huu, niwaagize wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya  kuwashughulikia kisheria watu wote wakataokwamisha utendaji wa viongozi wa serikali za mitaa,”alisema.

Alisema ni vizuri, viongozi wakatumia uongozi shirikishi kwa kusimamia maamuzi ambayo yametolewa na wananchi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwaonya kuacha kutumia ubinafsi katika utendaji wao wa kazi kwani kwa kufanya hivyo watapata wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yao.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Efreim Lema alisema  tangu viongozi hao wachaguliwe wamekuwa msitari wa mbele kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari.

“Tangu hawa viongozi wachaguliwe na kuapishwa, wamekuwa msitari wa mbele katika kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo maeneo yao,kila shule ya sekondari ya tunajenga vyumba vya madarasa ili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani wanaanza masomo na hakuna hata mtoto mmoja ambaye atabaki nyumbani,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles