23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Vijiji nchi nzima kupata umeme kufikia 2021

RAMADHAN HASSAN

Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini imedhamiria kufikisha umeme katika vijiji vyote visivyo na umeme nchini ifikapo Juni 2021.

Hayo yameelezwa bungeni leo Juni 18, na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Monduli Julius Laizer (CCM) aliyetaka alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka umeme katika shule ya Sekondari Oldonyolengai ambapo lami imefika toka mwaka 2015 lakini mpaka sasa hakuna umeme.

Akijibu swali hilo Subira amesema kulingana na mpango wa kupeleka umeme katika vijiji 64 wilayani Monduli, vijiji 16 vilishapatiwa umeme kupitia awamu ya pili ya miradi ya kusambaza umeme vijijini (REA-11), vikiwemo vijiji vya Arkatani na Mti.

Amesema kazi za mradi zinahusisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilometa 48.75 na njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 0.4 yenye urefu wa kilometa 40.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles