25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti kamati ya viwanda na biashara alia na tozo za TRA

Ramadhan Hassan-Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Seleman Sadiqq, amesema  ukadirio wa kodi unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na kutokuruhusiwa wafanyabiashara wanaonunua bidhaa China na Dubai kwenda na fedha taslimu umekuwa ni tatizo.

Akichangia mjadala wa Bajeti kuu ya Serikali leo June 18 bungeni Sadiqq amesema tatizo lipo kwenye ukadiriwaji wa kodi na kwamba biashara za Dubai na China zimetawaliwa kwa kulipa fedha taslimu.

“Ni muhimu kwa Benki Kuu (BOT), ueleze utaratibu wa kupeleka fedha taslimu ukoje. BOT wasaidie kuhakikisha biashara inarudi Kariakoo, kwa sasa imepotea katika ramani ya biashara,” amesema.


“Tulikuwa na Kariakoo ya wafanyabiashara kutoka Malawi, Kariakoo, Burundi, Congo, Uganda na Rwanda, BOT na TRA lazima wajiuelize kuna nini na sababu zipi tulizopoteza biashara Kariakoo,” amesema.


Aidha Mbunge huyo amesema sera ya Tanzania ya viwanda kwa sasa inatekelezeka kwa vitendo kutokana na ujenzi wa viwanda unaofanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles