24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

VAN VICKER: NDOA NI TAMU

ACCRA, GHANA


NYOTA wa filamu nchini Ghana, Joseph Van Vicker, mapema wiki hii alikuwa anasherehekea miaka 14 ya ndoa yake, hivyo amedai kuwa, ndoa ni tamu, hasa ukimpata mtu ambaye mnapendana.

Msanii huyo alianza uhusiano na Adjoa Vicker mwaka 1994 na baada ya muda kwenye uhusiano walifanikiwa kufunga ndoa ambayo imewafanya hadi sasa wafikishe miaka 14, hivyo msanii huyo amedai ndoa ni tamu endapo unampata mtu ambaye unapendana naye.

“Ni historia kubwa ya safari ya uhusiano wangu na Adjoa, miaka 23 sasa tangu tukutane na kuanza uhusiano, mapenzi ya kweli yametufanya tuwe hapa na kuiona ndoa tamu.

“Tuna furaha kubwa kusherehekea miaka 14 ya ndoa yetu, lakini sasa ni miaka 23 tangu tuanze uhusiano na tunaamini tutaendelea kudumu hadi mwisho wa maisha yetu,” alisema Van Vicker. Wawili hao wamefanikiwa kuwa na watoto watatu, wawili wakiwa wa kike.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles