23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

UVUVI WACHANGIA UTORO KWA WANAFUNZI

 

Na ANNA RUHASHA


IDADI kubwa  ya wanafunzi wa darasa la tano na  saba katika Shule ya Msingi Chifungu     katika  Halmsahuri ya  Buchosa  wilayani  Sengerema ,   wanajishughulisha  na   uvuvi hali inayochangia kuwa watoro shuleni, imefahamika.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,  Novatus Mtabi,  akizungumza kwenye mahafali ya darasa la saba,   alisema utoro umekuwapo shuleni hapo kwa muda mrefu kwa vile  baadhi ya wanafunzi hujishughulisha na   uvuvi.

Mtabi alisema wanafunzi wanaoongoza kwa uvuvi ni wa kiume wakati watoto wa kike wao hukimbilia visiwani na mijini ambako hujishughulisha na kazi za ndani  hali hiyo imekuwa ikiongeza utoro kwa   wanafunzi hao.

 Alisema mbali na changomoto hizo   shule hiyo pia inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ya kujifunzia  husasan madarasa kutokuwa na sakafu na nyumba za walimu na kutokuwapo maji  safi na salama.

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Sengerema,  Elizabeth  Kirumbu, ambaye alikuwa mgeni rasmi  katika  mahafali  hayo, aliwakumbusha wazazi na walezi  kufuatilia  maendeleo ya  masomo ya  watoto wao hatua inayosaidia  kujua  kama kuna changamoto  zinazowakabili .

“Niwaombe wazazi na walezi  kufuatilia maendeleo ya masomo ya watoto wenu.

“Hatua hii itasaidia kubaini mtoto wako ana changamoto zipi siyo kulipa ada tu halafu na kukaa, ukifuatilia mienendo ya masomo ya mwanao ni hazina tosha katika kumuandalia maisha bora, ”alisema Kirumbu.

Pia aliwaomba wazazi kuwafungulia akaunti za kuwatunzia fedha kidogo kidogo   watoto wao kusaidia kupunguza changamoto kwa wanafunzi kukatisha masomo kutokana na kukosa mahitaji muhimu  wakati akipata elimu.

Mmoja ya wanafunzi ambaye amekuwa mtoro   kutokana na kuvua samaki ambaye hakutaka  jina lake litajwe gazetini, alisema chanzo kikubwa cha kukatisha  masomo na kukimbilia visiwani ni   wazazi wao kutowatimizia mahitaji muhimu kama kuwapatia  sare za shule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles