24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI: JERAHA LA MCHANA HUPONA HARAKA KULIKO LA USIKU

LONDON, UINGEREZA


WANASAYANSI nchini Uingereza wamegundua majeraha yanayotokana na kujikata  au kuungua, hupona haraka yanapopatikana mchana ikilinganishwa na usiku.

Utafiti huo unasema seli za ngozi ya mwanadamu hubadilisha tabia yake kulingana na muda, huku protini zinazohitajika kurekebisha majeraha hayo zikifanya kazi vizuri wakati wa mchana.

Jeraha la moto nyakati za usiku lilichukua siku 28 kupona ikilinganishwa na siku 17 za jereha lililotokea mchana.

Watafiti walitaja tofauti hiyo kuwa kubwa, huku wakiongeza wanaweza kuharakisha watu kupona kwa kutumia dawa za steroids ambazo hubadilisha muda wa mwili.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la Sayansi, uliwahoji wagonjwa 118 katika kitengo cha wagonjwa walioungua nchini Uingereza.

Matokeo ya maabara yalionyesha kuwa seli za ngozi zijulikanazo kama Fibroblast zilikuwa zikibadili uwezo wake katika kipindi cha saa 24.

Seli hizo ndizo za kwanza zinazokimbia katika jeraha hilo ili kufunga kidonda.

Nyakati za mchana huwa zinafanya kazi zaidi na hupoteza nguvu hiyo usiku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles