24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 7, 2024

Contact us: [email protected]

MUGABE: MAKAMU WANGU ALIKWENDA KWA WAGANGA KUULIZA NITAKUFA LINI

HARARE, ZIMBABWE


RAIS Robert Mugabe amemlaumu makamu wake aliyemfukuza, Emmerson Mnangagwa, kuwa alikuwa akienda kwa waganga wa kienyeji kuulizia lini angekufa, limeandika gazeti la Serikali la Herald jana.

Mnangagwa, ambaye ameripotiwa juzi jioni kuikimbia nchi kwa kile alichoeleza kuwapo vitisho vya kuuawa, amekana tuhuma hizo na kusema hatua zilizochukuliwa dhidi yake, ni utekaji chama (Zanu-PF) uliofanywa na familia ya Mugabe.

“Mnangagwa awali alisambaza uvumi kuwa nilipanga kustaafu Machi mwaka huu, lakini baada ya kugundua hilo halikutokea, alianza kuwaendea waganga kuulizia lini nitakufa.

“Kisha akaenda katika kanisa moja la kimitume kujua ni lini Mugabe atafariki. Lakini huko aliambiwa atafariki yeye wa kwanza,” alisema Mugabe akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake mjini hapa juzi.

Mugabe mwenye umri wa miaka 93, alisema Mnangagwa alikosa maadili na alijaribu kuanzisha uasi ndani ya Zanu-PF.

Mwanzoni mwa wiki, Mugabe alimfuta Mnangagwa, mshirika wake wa karibu wa tangu vita vya uhuru vya miaka ya 1970, katika kile wadadisi wanasema ni njia ya kumwezesha mke wake Grace kuchukua madaraka wakati atakapofariki dunia au kustaafu.

Mugabe anatarajiwa kumteua Grace kuwa Makamu wa Rais katika mkutano utakaofanyika mwezi ujao.

Grace amekuwa akitoa wito wa kutaka kufukuzwa Mnangagwa kutoka chama cha Zanu-PF, ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1980.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles