Imechapishwa: Wed, Dec 6th, 2017

URUSI, IRAN KUONGEZA USHIRIKIANO

MOSCOW, URUSI


SERIKALI ya Iran imesema ina mpango wa kufanya mazungumzo zaidi na Urusi ili kuona uwezekano wa kuongeza ushirikiano zaidi katika nyanja ya uwekezaji.

Taarifa hiyo imetolewa juzi mjini hapa na Spika wa Bunge la Iran, Ali Larijani, ambaye alikuwa akihudhuria mkutano wa kimataifa wa kupambana na dawa za kulevya.

Alisema katika mpango huo wataandaa mfumo ndani ya mabunge ya nchi hizo mbili ambao utarahisisha uwekezaji.

“Tutafanya mazungumzo ya kusaidia ushirikiano katika uwekezaji kati ya Urusi na Iran, tutaandaa mfumo ndani ya Bunge letu utakaorahisisha kampuni kubwa kutoka Urusi kuwekeza nchini Iran,” alisema Spika huyo mara baada ya kukutana na Naibu Spika wa hapa, Sergei Neverov ambaye alimpokea uwanja wa ndege.

Kwa upande wake, Neverov alisema ni jambo  muhimu kwa wabunge wa nchi hii kujifunza kutoka kwa mataifa mengine jinsi wanavyokabiliana na tishio hilo la dawa za kulevya.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

FACEBOOK

YOUTUBE

Translate »

URUSI, IRAN KUONGEZA USHIRIKIANO