27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

UN YATUMA UJUMBE KOREA KASKAZINI

BEIJING, CHINA


UJUMBE wa Umoja wa Mataifa (UN) umeelekea mjini Pyongyang mchana wa jana kwa ziara yenye lengo la kujaribu kuzima mvutano kati ya taifa hilo na Marekani kufuatia mpango wa silaha za nyuklia wa Korea Kaskazini.

Mvutano mkali unaoendelea kati ya Marekani na Korea Kaskazini kutokana na mpango wake wa silaha za nyuklia, unaendeleza hali ya wasiwasi katika eneo la Korea na duniani kwa ujumla.

Kutokana na hali hiyo, UN imetuma ujumbe wake ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayehusika na masuala ya siasa, Jeffrey Feltman kwenda Korea Kaskazini kujaribu kutuliza hali.

Ziara ya Feltman, ni ya kwanza kufanywa na mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa umoja huo tangu mwaka 2010.

Haya yanajiri siku chache baada ya Korea Kaskazini kusema imefanikiwa katika jaribio la kombora jipya linaloweza kufikia Marekani.

Aidha inakuja siku moja baada ya Marekani na Korea Kusini kuanza mazoezi ya pamoja na  kijeshi, kuonyesha utayari wa kukabiliana na kitisho cha Korea kaskazini.

Kabla ya kutua nchini humo, Feltman, alipitia China ambako alikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China mjini Beijing.

China, ambayo ni mshirika pekee wa kidiplomasia na kijeshi wa Korea Kaskazini, imetoa wito kwa Marekani kusitisha mazoezi hayo, na kumtaka pia mshirika wake asitishe ili kutuliza hali  hiyo tete.

Msemaji wa UN, Stephane Dujarric, alisema kuwa Feltman akiwa Korea Kaskazini, atajadili juu ya  ‘maswala ya masilahi ya pamoja na yenye umuhimu zaidi’ na viongozi wa taifa hilo la kikomunisti na kukutana na kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jung-Un.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles