28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Uhaba wa viwanja chanzo kupotea kwa vipaji vya michezo

Glory Mlay

Ni rahisi kuwaona watoto au vijana wakicheza soka mitaani.

Hii ni kwasababu, angalau vipo viwanja vichache vinavyoweza kutumika kwa mchezo huo.

Lakini ni vigumu kuwaona watoto au vijana wakicheza michezo mingine kama tenisi, netiboli, wavu na mpira wa meza tofauti kutokana na uhaba wa viwanja vya michezo husika.

Hili hii haiishii mitaani, bali hata kwenye shule.

Ni shule chache tu zinazomiliki  viwanja vya michezo hiyo.

Jambo la kushangaza ni michezo ambayo ni rahisi kuwa kutengeneza viwanja vyake.

Ukiondoa mpira wa meza, wavu na netiboli inahitaji magoli ambayo ya chuma, nyavu na mipira, hata hivyo bado haina viwanja vya kutosha mitaani.

MTANZANIA limefanya mahojiano na viongozi wa vyama vya mpira wa wavu, mikono, meza, tenisi na netiboli na hapa wanafunguka kuhusu changamoto ya viwanja.

Judith Ilunga

Ni Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta).

Anasema ni rahisi mchezo huo kuchezwa mitaani kwani mbali ya eneo la kuchezea (uwanja) kingine kinachohitajika ni nguzo mbili za chuma kwa ajili ya magoli na nyavu.

Anasema vifaa hivyo vikiwepo mchezo huo unaweza kuchezwa hata kama uwanja utakuwa umechorwa na chaki tu.

Anasema changamoto ya ufadhili ndiyo inayokwamisha mchezo huo kuchezwa kila mahali.

“Magoli ni kazi rahisi kupatikana, siwezi kusema kwa nini nyuma ilishindikana kuchezwa kila mahali, lakini sasa nataka netiboli ichezwe hadi kwenye kata,” anasema.

Anasema katika uongozi wake watahakikisha wanalifanyia kazi hilo ili kuona mchezo huo unachezwa kila mahali.

“Watu wajue netiboli ipo kila kona ya Tanzania kuanzia kwenye shule, vijijini, kata, mikoa hadi taifa,”anasema.

YUSUFU MKARAMBATI

Ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es Salaam (Dareva).

Anasema mchezo huo hata katika uwanja wa nyasi unachezwa, kinachohitajika ni vyuma viwili, mpira wa kuchezea na nyavu za magoli.

Anasema ni vigumu kueleza kwa nini mchezo huo hauchezwi mitaani na hakuna viwanja vyake wala klabu za kiraia.

Mkarambati anasema wanafikiria kutafuta maeneo ya kujenga viwanja vya mchezo huo mitaani.

Anasema mchezo huo nchini unachezwa hasa na timu za majeshi, lakini mfumo wa kupata wachezaji wao unakuwa mgumu.

Anasema baadhi ya shule zinazotoa mafunzo ya mchezo huu lakini changamoto ikiwa viwanja.

SALUM MVITA

Ni kocha wa timu za vijana za mchezo wa tenisi hapa nchini.

Anasema  watu wengi  wamejenga taswira kuwa mchezo huo unachezwa na watoto waliotokea kwenye familia bora.

Anapingana na hisia hizo kwa kusema kila mmoja anaweza kucheza tenisi.

Haya hivyo ni wazi kuna uhaba wa viwanja vya mchezo huo.

Vichache kama kile cha Klabu ya Gymkhana na Chuo cha Posta vinavyopatikana jijini Dar es Salaam vinalipisha ada kwa mtu anayetaka kujifunza mchezo huo.

Uwanja wa tenisi unahitaji vyavu, vyuma viwili kwa ajili ya magoli, mipira na racket(kifaa maalumu ya kupigia mpira).

Mvita anasema ni rahisi mno kuwa na viwanja vya tenisi, lakini ni vigumu kupata vifaa vya kuchezea.

“Ugumu upo katika vifaa kwani vinauzwa bei kubwa.

Inatuwia ugumu sisi kama chama kuweka magoli sehemu yoyote,” anasema Mvita.

Mvita anasema kwa sasa wanajaribu kuupeleka mchezo huo kwenye shule pamoja na kutoa vifaa licha ya kwamba havitoshelezi.

ISSA MTALASO

Ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Meza Tanzania (TTTA).

Anasema wameandaa mpango maalumu wa kuhakikisha mpira wa meza unachezwa kwenye shule zote hapa nchini.

Anasema ugumu siyo kuwa na maeneo ya kuchezea mpira wa meza bali vifaa.

Anatolea mfano meza ambazo hutumika kwa ajili ya mchezo huo kwa kusema zinauzwa bei ghali.

“Pia racket ya kuchezea ni gharama kubwa hivyo inatuwia vigumu kuupeleka mchezo huu kila mahali japo tuna mikakati hiyo.

Tunachofanywa kwa sasa ni kuupeleka kwenye shule za Dar es Salaam,” anasema Mtalaso.

Mnonda Magani

Ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es Salaam (DRHA).

Anasema changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni ukosefu wa viwanja vya kufanyia mashindano.

Anasema viwanja vilivyopo vimejaa mashimo na kuwafanya wachezaji washindwe kucheza.

“Changamoto ya viwanja ni tatizo kubwa kwetu hasa kwa wakati huu ambao wachezaji ni wengi.

“Vinavyotumika kwa sasa havina ubora kwa sababu vimejaa mashimo,” anasema.

Magani anaiomba serikali kuwatengenezea maeneo yao.

“Wachezaji ni wengi na sisi tunaendelea kukuza na kuendeleza vipaji vya mchezo huu hivyo tunahitaji maeneo yakuwafunzia.

“Viwanja vilivyopo hatuvitumiki kwa uhuru kwa sababu wachezaji wa michezo mingine pia wanavitumia.

“Tunatakiwa kuwa na viwanja vyetu sisi wenyewe kama ilivyo soka,” anasema Magani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles