23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

UFARANSA YAKATAA KUITAMBUA CATALONIA

PARIS: Ufaransa

SERIKALI ya Ufaransa imesema haitambua Catalonia ikijitangazia uhuru kutoka kwa Hispania na kwamba hatua hiyo itasababisha ifukuzwe kutoka kwenye Umoja wa Ulaya (EU).

Waziri wa Masuala ya Ulaya wa Ufaransa,   Nathalie Loiseau amesema mgogoro huo uliosababishwa na kura ya kutaka iwe huru iliyopigw na Catalonia Oktoba mosi na ambayo Hispania iliipiga marufuku, unapaswa kutafutiwa ufumbuzi kwa njia ya mazungumzo.

“Kama ikijitangazia uhuru, sisi hatutaitambua hatua hiyo,” alisema   Loiseau.

“Athari ya kwanza itakuwa nikufukuzwa kwenye  Umoja wa Ulaya.”

Rais wa Catalonia,  Carles Puigdemont, anatarajia kulihutubia bunge la jimbo hilo leo.

Hadi sasa jimbo hilo halijafikia maafikiano yoyote na Hispania.

Habari zinasema huku vuguvugu la uhurulikizidi Catalonia, kampuni nyingine tatu zilitarajiwa kujadili kuondoa ofisi zao jiboni humo.

Kampuni hizo ni Abertis inayohusika na masuala ya miundombinu, Cellnex  inayohusika na masuala ya   mawasiliano  na kampuni ya Inmobiliaria Colonial inayoshughulikia  masuala ya bidhaa.

Kampuni kubwa za Caixabank na Sabadell  zimekwisha kutangaza kuhamisha ofisi zao kutoka katika jimbo hilo.

Jimbola Catalonia lenye wakazi milioni 7.5, kaskazini mashariki mwa Hispania, ni muhimu kwa nchi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa katika nchi wanachama wa EU na mwanachama wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles