TYRESE, DWAYNE WALIANZISHA BIFU JIPYA

0
6

NEW YORK, MAREKANI


NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Tyrese Gibson, amelianzisha bifu jipya kwa kumwambia mkali wa filamu ya Fast & Furious, Dwayne Johnson ‘The Rock’ kuwa ni mbinafsi sana.

Wawili hao ni marafiki wakubwa kutokana na filamu hiyo, lakini kwa sasa wanaonekana kuwa kwenye mgogoro kutokana na ucheleweshaji wa kuachia kwa filamu yao nyingine.

“The Rock ninaamini ana ubinafsi sana, kuna mambo yetu ya pamoja anaamua kuyafanya kimya kimya jambo ambalo si zuri, yupo vizuri kwenye kazi lakini ana mapungufu yake makubwa sana.

“Sina ugomvi naye lakini lazima niseme ukweli, Fast and Furious 9 ilitakiwa kutoka hivi karibuni lakini imesitishwa hadi 2020,” alisema Tyrese.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here