23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

TASAF YAANZA KUTOA MALIPO KWA NJIA YA MTANDAO

Na AMON MTEGA -SONGEA

HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, imeanza kutoa malipo kwa njia ya mtandao kwa kaya masikini 4,959 zilizopo katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf).

 Mratibu wa Tasaf katika Manispaa ya Songea, Christopher Ngonyani, alisema wanufaika wa Tasaf wapatao 604 wamejisajili kulipwa kwa njia ya mitandao ya simu kati yao wanufaika 475 wameingiziwa fedha zao katika malipo ya Julai-Agosti mwaka huu.

Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa wanufaika wote wa Tasaf wanaingizwa kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao kwa kuwa yanalipwa moja kwa moja na Tasaf kutoka makao makuu badala ya fedha kutumwa katika halmashauri hivyo kutumia muda mrefu hadi kuwafikia walengwa.

“Jumla ya Sh milioni 16.5 zimelipwa wiki hii kwa kaya masikini  475 moja kwa moja kutoka makao makuu na tayari kaya hizo zimepata fedha zao kwa njia ya mitandao ya simu zao na wale ambao hawajasajiliwa bado hawajalipwa,” alisema.

Hata hivyo, alisema kaya 4,484 ambazo bado hazijasajiliwa malipo kwa mtandao wa simu zitalipwa fedha zao kwa njia ya fedha taslimu kuanzia wiki ijayo ambapo zaidi ya Sh milioni 155.9 zitalipwa kwa wanufaika hao.

Ngonyani alisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha wanufaika wote wa Tasaf wanajisajili kulipwa kwa njia ya mitandao ya simu ili kuepukana na changamoto nyingi ambazo zimejitokeza katika malipo ya fedha taslimu ikiwemo kutolewa malipo hewa.

Watendaji wa Tasaf Manispaa ya Songea kwa kushirikiana na watendaji wa Tasaf kutoka makao makuu kitengo cha malipo kwa njia ya mtandao wanatembelea katika mitaa ya wanufaika katika manispaa hiyo ili kuangalia changamoto zilizojitokeza katika mfumo mpya wa malipo kwa njia ya mtandao pia kuwahamasisha wananchi kujisajili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles