29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA RUNGWE WATISHIA KUACHA KULIMA ZAO LA CHAI

Na PENDO FUNDISHA

-MBEYA

WAKULIMA wa zao la chai wilayani Rungwe, mkoani Mbeya, wametishia kung’oa miche ya zao hilo na kupanda  tunda la parachichi mara msimu wa kilimo utakapoanza.

Wamesema zao hilo limeonekana kutomnufaisha mkulima hivyo ni vema wakaachana na kilimo hicho na kuzalisha  tunda la parachichi ambalo kwa sasa limeonekana kuwa na tija.

Wakulima hao wa Kata ya Kyimo, wilayani Rungwe, waliyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla.

Walisema wamefikia uamuzi huo, baada ya  kuchoshwa na vitendo vya ukiritimba wa ununuzi wa zao la chai nchini, hivyo wamepanga kutoendelea na kilimo hicho kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuondoa mfumo kandamizi unaodaiwa kufanywa na bodi ya chai.

“Tumegoma kuuza chai yetu kwa Kampuni ya Kiingereza ya WATCO na kifupi tunang’oa chai na kupanda zao la parachichi,” haya ni baadhi ya maneno yaliyokuwa yameandikwa kwenye mabango yaliyokuwa yamebebwa na wananchi.

Walisema mfumo huo umeghubikwa na changamoto za kisheria hasa kwenye suala la ununuzi wa zao hilo kwa kutoruhusu kuwepo kwa ushindani wa kisoko hivyo mkulima kulazimika kuuza zao hilo kwa mnunuzi mmoja na kwa bei takwa.

Akizungumzia changamoto hizo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Makalla, alisema Serikali imeliona tatizo hilo na kwamba tayari kamati maalumu iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, kwa ajili ya kuchunguza malalamiko hayo imewasili jijini hapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles