24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru yachunguza miradi ya Sh bilioni 1.24

Damian Masyenene – Shinyanga

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Shinyanga, inafuatilia miradi tisa ya maendeleo inayopewa fedha za Serikali na ufadhili wa wadau wa maendeleo iliyogharimu Sh bilioni 1.249 kujiridhisha kama matumizi yake yanalingana na maelekezo yaliyotolewa.

Katika taarifa ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2019/20  iliyotolewa na Takukuru mkoani hapa, iliitaja miradi hiyo kuwa ni Elimu (5), Barabara (2) na afya (2) ambayo matumizi ya fedha katika miradi hiyo yanafanyiwa uchambuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Takukuru Shinyanga, Kaimu Mkuu taasisi hiyo, Hussein Mussa alisema uchambuzi wa kina katika matumizi ya fedha hizo unaendelea na itakapobainika kuna ubadhirifu sheria itachukua mkondo wake.

“Miradi ya barabara ina thamani ya Sh milioni 676.98, elimu Sh milioni 367.9 na afya Sh milioni 204.4 zote hizi tunazifuatilia na tunafanya uchambuzi wa kina katika matumizi yake,” alisema Mussa.

Takukuru pia ilifanikisha kuokoa Sh milioni 30.5 za wakulima wa pamba zilizotafunwa na viongozi wa AMCOS ambao wamekubali kuzirejesha na zitagawiwa kwa wakulima hao.

Alisema fedha hizo ni sehemu ya Sh milioni 103.134 zinazodaiwa na wakulima 331 wa pamba mkoani Shinyanga zilizofujwa na viongozi wa Amcos za Ng’washinong’hela, Nyenze, Lagana, Kalitu, Muhunze na Ibadakuli.

Katika hatua nyingine Mussa alibainisha kuwa kwa kipindi cha Oktoba – Desemba mwaka jana, Takukuru ilipokea taarifa 69 ambazo baadhi yake uchunguzi umekamilika, huku kesi 20 zikiendelea mahakamani zikiwemo tisa za Serikali za mitaa, tatu za idara ya afya, elimu (3), uhamiaji (2), sekta binafsi (1), idara ya michezo (1) na mahakama kesi moja.

“Kwa mujibu wa taarifa tulizopokea idara zinazolalamikiwa ni Serikali za mitaa (48), polisi (19), elimu (8), vyama vya siasa (9), mahakama (7), sekta binafsi (5), afya (4), ardhi (3), ushirika (2), TRA (2), Tasaf (2), kilimo (1), michezo (1), dini (1), maji (1), Tarura, Ushirika na bima wote wakiwa na kesi moja kila mmoja,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles