24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Stamina atoa somo ndoa yake kuvunjika

Christopher Msekena

MIAKA mitatu iliyopita staa wa Hip hop, Boniventure Kabogo ‘ Stamina’, akiwa kwenye kazi zake alikutana na Veronica Peter, binti mwenye asili ya Kinyarwanda aliyekuwa anafanya mafunzo kwa vitendo (field) katika kituo fulani cha redio jijini Dodoma.

Mchizi alisaka mawasiliano ya mrembo huyo mpaka akayapata na  hapo ndipo mapenzi yao yalipoanza na ndani ya muda mfupi yalifika hatua kubwa ya kutambulishana kwa ndugu zao  ambao wengi wanaishi mkoani Morogoro.

Desemba 11, 2017, Stamina alipiga goti na  kuuliza lile swali maarufu kwa kimombo, ‘Will you marry me?’ na akamvisha pete ya uchumba mrembo huyo tayari kuingia kwenye maisha mapya ya ndoa.

Mei 5,  mwaka juzi alifanikiwa kufunga ndoa na Veronica katika kanisa la Mtakatifu Consolata huko SUA, Morogoro  mbele ya wasimamizi wao ambao ni rapa Roma Mkatoliki na mke wake Nancy.

Kwa mujibu wa Roma anasema ndoa hiyo ilivunjika rasmi   mwaka jana mwezi Februari baada ya mke wa   Stamina    kuondoka nyumbani licha ya kufanyika kwa vikao vingi vya ushuruhishi ndoa hiyo iliendelea kupumlia mipira.

Roma anasema ingawa  Veronica kuwa na mapungufu ila Stamina naye alikuwa na matatizo yake ambayo ni kawaida kuwapo ndani ya ndoa nyingi kutokana wanandoa kuwa ni bi binadamu wenye madhaifu yao.

Mapema juzi, Stamina alichia ngoma yake, Asiwaze ambayo sasa hivi imeshika namba moja katika video zinazotazamwa zaidi YouTube. Ndani ya wimbo huo ametumia sanaa ya uandishi kuelezea matatizo ya ndoa yake huku akitaja usaliti ndiyo chanzo kikubwa cha kuvunjika kwa ndoa yake.

Stamina alimtumuhu mkewe kuchepuka na aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Simba ambaye hakutaka kumuweka wazi jambo lililofanya ndoa yake kuvunjika ikiwa haijafikisha hata mwaka.

Katika hilo Stamina ametoa ushauri kwa vijana wanaotarajiwa kuingia kwenye ndoa pamoja na wazazi wenye watoto wenye mipango ya kufunga pingu za maisha.

“Mnavyoingia kwenye ndoa mnakutana watu kutoka familia tofauti, tabia tofauti, malezi tofauti mpaka kuja kuelewana na kuwa kitu kimoja inachukua muda, kwahiyo uchumba inatakiwa uwe mrefu angalau miaka mitano.

“Siyo mapenzi ya mbali yaani babe yupo Mwanza wewe upo Dar, mkikutana lazima utaigiziwa tu, utaona daaah mwanamke ana heshima huyu kumbe heshima yenyewe umeonyeshwa  mara nne tu,” anasema Stamina.

Aidha Stamina aliongeza kuwa: “Wapenzi nawashauri wapate muda mwingi wa kuwa pamoja ili waweze kujuana, huyu ana tabia hii yule ana tabia ile harafu ikiwezekana wazazi waruhusu kabla ya ndoa watoto wakae hata mwaka tu ndani ili wasomane.

“Mimi sikuwahi kuishi naye kabla ya ndoa, tulikuwa tunakutana tu  kisha anarudi nyumbani siyo ile pika pakua pika pakua ya muda mrefu ndiyo naama nashauri sana iwe  hivyo sababu inasaidia kujuana vizuri.”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles