26.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Simba na Mwadui tena, Yanga, Prisons kazi ipo

Theresia Gasper -Dar es salaam

TIMU ya Simba imepangwa kucheza dhidi ya Mwadui, katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya michuano ya Shirikisho maarufu Kombe la Azam, huku Yanga ikipewa Tanzania Prisons, michezo itakayochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, kati ya Januari 24 na 26 mwaka huu.

Simba ilitinga hatua hiyo, baada ya kuifunga Arusha FC mabao 6-0, wakati Yanga ikiifunga Iringa United mabao 4-0, michezo iliyopigwa dimba la Uhuru.

Mshindi kati ya mchezo kati ya Simba na Mwadui, atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Majimaji na Stand United.

Naye mbabe kati ya Yanga na Prisons atakutana uso ka uso na mshindi kati ya  Gwambina na Ruvu Shooting, katika hatua ya 16 bora.

Mwadui iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza na pekee mpaka sasa kuifunga Simba msimu huu ilipoitungua bao 1-0, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa Ocktoba 30 mwaka jana, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Kwa upande mwingine Yanga ilikuwa timu ya kwanza msimu huu kuifunga Prisons ilipoilaza bao 1-0, katika mchezo  uliorindima dimba la Samora, Iringa.

Kulingana na droo hiyo iliyochezeshwa jana, mabingwa watetezi wa michuano hiyo, timu ya Azam itakipiga na Friends Rangers Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, wakati Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa Might Elephant kwenye dimba la Kaitaba, Kagera.

Azam imefika hatua hiyo, baada ya kuifunga African Lyon mikwaju ya penalti 4-1, baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Sahare All Stars Uwanja wa CCM Gairo, Namungo FC itawakaribisha Biashara United dimba la Majaliwa Lindi.

Lipuli itataumana na Kitayosa FC ya Tabora dimba la Samora, Iringa wakati JKT Tanzania itakuwa mwenyeji wa Tukuyu Stars ya Mbeya Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo, Dar es Salaam.

Ruvu Shooting itapepetana Gwambina dimba la Gwambina Mwanza, Alliance itakuwa mgeni wa African Sport Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Mbeya City itapimana ubavu na Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika,  Moshi huku Ndanda ikiwa mwenyeji wa Dodoma Jiji dimba la Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Majimaji itatoana jasho na Stand United Uwanja wa Majimaji Songea, Gipco ya Geita itatunishiana msuli na Ihefu ya Mbeya.

KMC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa ya Pan African Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wakati Panama itavutana mashati na Mtwiliva.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles