Imechapishwa: Wed, Sep 13th, 2017

SPIKA NDUGAI: ZITTO ACHA KUNICHEZEA

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), kuacha kumchezea kwani anaweza kumzuia kuongea bungeni hadi atakapomaliza muda wake wa ubunge.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo bungeni leo Septemba 13, ambapo pia ameiagiza tena Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge, kumuita na kumhoji Zitto baada ya kuendelea kutoa kauli za kulidhalilisha Bunge.

Jana, Spika Ndugai aliagiza kamati hiyo kumhoji Zitto kuelezea ni kwanini alimlaumu Spika juu ya uamuzi wake wa kamati za almasi na tanzanite kutojadiliwa bungeni badala yake kuwasilishwa serikalini wiki iliyopita.

Baada ya kuagizwa kwa kamati hiyo na Spika jana, Zitto aliandika ujumbe tofauti katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, akikubali wito huo wa Spika kwa kamati na kuelezea namna anavyoshangazwa na mwenendo wa Spika katika kuliendesha Bunge huku akiingiliwa na mhimili mwingine.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

SPIKA NDUGAI: ZITTO ACHA KUNICHEZEA