24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Shibuda azidi kuwasuta vigogo wafitini

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KATIBU Mtendaji wa Chama cha Ada-Tadea, John Shibuda kwa mara nyingine amewarushia kombora viongozi wastaafu ambao wamekuwa wakikosoa misingi ya CCM chini ya Rais Dk. John Magufuli.

Amesema suala la kuibuka kwa msamiti wa ‘CCM ya Magufuli’   inaonyesha maana halisi ya kaulimbiu ya ujenzi wa CCM madhubuti yenye maono halisi kwa Watanzania.

Alikuwa akizungumza   Dar es Salaam jana kuhusu hali ya siasa nchini.

Shibuda  alidai  kauli ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kupinga kuitwa kwa CCM ya Magufuli  ni wazi inakwenda kinyume na misingi na kaulimbiu za maendeleo ambayo Tanzania sasa inapitia.

“Ni utamaduni wetu tulizoa kwamba nchi kutoka kwa mgombea CCM kila baada ya miaka 10.

“Na tulipokea duru za siasa na rai za wito wa ahadi za dhana iliyobeba dhima iitwayo, Magufuli for Change, hii ni katika ahadi za wagombea urais wa Tanzania mwaka 2015.

“Vivyo hivyo ulikuwapo mfumo wa ahadi iliyoitwa Movement for Change ambayo si ahadi ya mgombea bali ni mfumo.

“Kwa hiyo sasa jamii na taifa lipo katika safari ya neema ya ahadi za kaulimbiu na dhima ya kusimamiwa dhana hii iitwayo Magufuli for Change ambayo ilitakiwa ithaminike na isadikike kwa vielezo vya ushahidi wa matokeo na vitendo,” alisema.

Alisema kwa Tanzania kulikuwapo hali ya matokeo ya athari za hali duni na udumavu na kuchangia kubomoka kwa maadili ya usalama na uhai wa manufaa yenye tija kwa ustawi na maendeleo ya jamii na  uchumi wa taifa.

Shibuda ambaye aliwahi kuwa mbunge wa CCM na baadaye Chadema mwaka 2010, alisema   historia ya utumishi wa Serikali ya Awamu ya Tano imeibua na kudhibiti kuwapo hali ya makundi ya wanaodhulumu rasilimali za taifa na wale wanaojukumu mapato ya nchi.

“Kwa hali hiyo sasa, uongozi wa mkuu wa awamu ya tano ni vema ukapokelewa vema na watu wote wa makundi na rika mtambuka wakiwamo wadau wa siasa za vyama vyote  kulisaidia taifa letu.

“Ni wazi huu kwetu ni mtaji wa kutengeneza mazingira rafiki yenye sifa ya uwajibikaji mwema na tiifu kwa uamifu wa CCM na uaminifu wa Serikali yake. Ni vema serikali iwe daima ni somo la kutimiza majukumu ya uzalendo kwa masilahi ya jamii, uchumi na taifa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles