24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuliweka kwenye kumbukumbu gari la Nyerere lililoundwa na Veta

Susan Uhinga, Tanga



Serikali imesema italichukua na kulihifadhi kama kumbukumbu ya vitu alivyokuwa anatumia hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, gari alilokuwa akitembelea mwaka 1968 na kuundwa upya na Chuo cha Ufundi Stadi (Veta), mkoani Kilimanjaro.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ally Mohamed Shein, amesema hayo jana katika sherehe za  kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru baada ya kutembelea banda la Veta na kujionea gari alilokuwa akitumia mwalimu wakati wa harakati zake za kutafuta uhuru ambapo pia aliwapongeza vijana hao kwa umahiri wa kutengeneza gari hilo.

“Vijana hao wameonyesha kwamba wamefuzu vizuri na wameonyesha uzalendo, Serikali inatambua mchango huo.

“Serikali itaongeza vyuo vya ufundi Tanzania Bara na Visiwani kwa lengo la kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kujiunga na vyuo hivyo ili waweze kujiajiri,” amesema Dk. Shein.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles