SERENGETI KUVAANA NA RWANDA LEO

0
399

NA MWANDISHI WETU


TIMU ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, leo inatarajiwa kucheza na Rwanda katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Afcon U-17).

Mchezo huo utakuwa wa tatu kwa Serengeti Boys kucheza katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Agosti 17, mwaka huu, Serengeti Boys waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Burundi.

Timu hiyo ilipata ushindi mwingine wa mabao 5-0 Sudan, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Fainali za Afcon U-17 inatarajiwa kuchezwa mwakani nchini, ambapo timu itakayoibuka mabingwa katika michuano ya  Cecafa, itaungana na Serengeti Boys ambayo imefuzu moja kwa moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here