24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

RIHANNA KUPEWA MTAA BARBADOS

CARIBBEAN, BARBADOS


WAZIRI wa Utalii wa Barbados ametangaza kuwa serikali ya nchi hiyo inatarajia kumpa mtaa nyota wa muziki wa pop nchini Marekani, Robyn Fenty, maarufu kwa jina la Rihanna.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 29, aliyezaliwa Barbados na kukulia mji wa Bridgetown, anatarajiwa kupewa mtaa huo katika kuadhimisha siku yao ya uhuru.

“Serikali ya Barbados itakuwa na maadhimisho ya siku ya uhuru Novemba 30, 2017, hivyo inatarajia kubadili jina la mtaa wa Westbury New Road, ambao upo St. Michael na badala yake kuitwa Rihanna Drive,” taarifa hiyo ilitoka Wizara ya Utalii ya Barbados.

Msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, alionesha kuwa na furaha baada ya kupokea taarifa hiyo na kudai kuwa, yupo tayari kuwapa burudani mashabiki wake siku hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles