24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

RC MTAKA AKARIBISHA WAZAWA KUWEKEZA SIMIYU

Na SAMWEL MWANGA,

WAFANYABIASHARA wazawa mkoani Simiyu wametakiwa kuwekeza katika sekta ya viwanda huku Serikali mkoani humo ikieleza kuwa iko tayari kuwaunga mkono.

Mkoa wa Simiyu umejipambanua kutekeleza azma ya Rais Dk. John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda, kwa kuanzisha viwanda kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza fursa za biashara na   kilimo.

Hayo yalielezwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka katika ufunguzi wa Jukwaa la Biashara la mkoa huo lililofanyika mjini Bariadi.

Liliandaliwa  na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Alisema   takriban fursa 14 zimetangazwa katika maeneo mbalimbali baada ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Uchumi na Jamii (ESRF) ulioandaa rasimu ya mwongozo wa uwekezaji wa mkoa.

“Tunataka kutafsiri Mkoa wa Simiyu na kuufanya kuwa wa tofauti katika kuelekea kwenye uchumi wa kati tungehitaji kujenga mkoa tofauti na watu wengine waje kujifunza hapa.

“Yapo tuliyoanza kutekeleza na yapo yaliyo kwenye maandalizi na mifumo imekamilika,” alisema.

Alisema hakutakuwa na urasimu   kwa mwekezaji yeyote ambaye atahitaji kuwekeza katika mkoa huo huku akiwataka  wakurugenzi wahalmashauri zote mkoani humo kutokuwa vikwazo katika kutekeleza azima hiyo.

Alisema  mkoa huo umeanzisha mfumo tofauti wa kushirikisha sekta binafsi katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda.

RC alisema mkoa  umeanza kwa halmashauri kuendesha viwanda vidogo kwa ubia na vikundi vya vijana ikiwamo wilaya ya Meatu (kiwanda cha kusindika maziwa) na Wilaya ya Maswa (Kiwanda cha Kutengeneza Chaki).

“Serikali mkoani hapa imedhamiria kuwa na viwanda vya kati na vikubwa kwa lengo la kuyaongezea thamani mazao ya kilimo na mifugo na yanayozalishwa  wakulima waone tija ya kilimo na ufugaji,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mtaalam wa masuala ya biashara, Profesa Elisante ole Gabriel aliwataka wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari  biashara zao ziwe endelevu kuliko kusubiri kufuatiliwa na serikali.

Naye Mhariri Mtendaji wa Kampuniya Magazeti ya Serikali (TSN), Dk. Jim Yonazi alisema kampuni yake inaamini maendeleo ni habari hivyo iko tayari kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu kwa kuwa viongozi wake wanachukia kasi ndogo katika maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles