30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

ASKOFU MBELWA AAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

Na KAHINDE KAMUGISHA,   

ASKOFU Mteule Godfrey Mbelwa wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Lweru mkoani Kagera, ameahidi kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika juhudi zake za kupambana na dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kuhimiza kufanya kazi.

Alikuwa akizungumza  katika ibada ya shukrani baada ya kusimikwa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Lweru Februari 5, mwaka huu.

Mbelwa alisema serikali ya awamu ya tano imejielekeza katika kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kupambana na uhalifu ukiwamo utumiaji wa dawa za kulevya.

Alisisitiza atatoa ushirikiano  na kuisimamia dayosisi yake kuongeza shule za sekondari  kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kusaidia jitihada za serikali.

“Tunatambua elimu ndiyo msingi wa maisha kwa wananchi wetu na jamii kwa ujumla.

“Hivyo ombi letu kwa Serikali ni kusaidia kuondoa migogoro ya ardhi kati ya Dayosisi na Kijiji cha Katoke ili kuendelea kuwaletea watanzania manufaa kupitia elimu na kuongeza fursa za ajira kwa vijana wetu,” alisema.

Alisema mkakati mwingine wa dayosisi hiyo kwa kushirikiana na wahisani ni kuwekeza katika  miradi ya kilimo cha kisasa  watanzania wapate lishe ya chakula bora na ajira kwa viwanda vya mazao ya kilimo na kuboresha huduma nyingine za jamii kama afya maji na utunzaji wa mazingira.

Dayosisi ya Lweru ilianzishwa mwaka 2006 baada ya  kugawanywa kwa Dayosisi ya Kagera ikiwa na dinari tatu, parishi 12 na makanisa 37 .

Mwaka huu inaelezwa kuwa na dinari nane,  parishi 38 na makanisa 119 yenye wachungaji 42 tofauti na wachungaji 13 wa awali.

Askofu Buberwa  alikuwa Katibu Mtendaji wa Dayosisi ya Kagera akisaidiana na Askofu wa Dayosisi hiyo, Dk. Aaron Kijanjali ambaye anatarajia kustaafu mwaka huu.

Mwaka 2006 alikuwa mchungaji Kanoni wa Dayosisi ya Lweru akiishi makao makuu Anglikana mkoani Kagera mjini Muleba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles