MOSCOW, Urusi
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin jana aliadhimisha siku ya kutimiza miaka 66 ya kuzaliwa kwake ambapo aliitumia kupumzika karibu na ndugu wa familia, marafiki na wasaidizi wake.
Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa Ikulu ya hapa, Dmitry Peskov wakati wa mahojiano na Shirika la Habari la nchi hii, TASS tofauti na walivyo viongozi wengine ambao huwa wanafanya sherehea kubwa kiongozi huyo huwa anaitumia siku hiyo kwa kupumzika huku akipokea ujumbe mbalimbali wa kumtakia kila la kheri.
Alisema kuwa kama jana kiongozi huyo alipokea salamu mbalimbali kutoka kwa viongozi wan je na miongoni mwa waliompigia simu ni Rais wa Belarusi, Alexander Lukashenko, Rais wa Azerbaijani, Ilham Aliyev na wa Armenia, Armen Sarkissian.
Alisema kwamba pia Waziri Mkuu, Dmitry Medvedev alimpigia simu Rais Putin akimtakia afya njema na mafanikio makubwa kwa kazi anayoifanya kwa ajili ya maslahi ya wananchi wan chi hii.
Mwaka jana Rais Putin aliitumia siku hiyo akiwa nje ya mji huu ambapo aliamua kukutana na maofisa wa Baraza la Usalama mkutano ambao ulifanyika mjini Sochi.
Mwaka 2016, pia Rais Putin aliitumia siku kama hiyo bila kufanya shughuli yoyote ikiwa ni baada ya mwaka mmoja kwenda kushuhudia mechi ya mpira wa magongo na huku mwaka 2014 akiisherehekea akiwa ziarani nchini Siberian.