24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

NMB YAUNGA MKONO DHANA YA MIRADI MIKUU KWENYE UCHUMI

Mwandishi Wetu


NI mabadiliko yanatokea kwa polepole ambayo ni mwafaka ingawa yamechelewa kufanywa na kwa kiasi kikubwa yanakosa uwazi wa kutoa mwelekeo kwa wadau bali hutumika hisia kuuona ukweli na  baada ya kufanya uchambuzi wa kina.

Baada ya kusuasua kiasi cha kuishawishi Serikali kuchukua hatua, wachambuzi wanaamini sekta ya fedha itaimarika zaidi mwakani na kuchangia ukuaji wa uchumi na Pato la Taifa (GDP) kama kila mdau atachukua hatua kwa furs zinazojitokeza.

Kutokana na mabadiliko kadhaa yaliyofanywa na serikali kuanzia mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, taasisi za fedha hasa benki za biashara ziliyumba.

Miongoni mwa athari  zilizojitokeza kutokana na  sera tatanishi za serikali ni kupungua kwa ukwasi  na hivyo kushuka kwa upatikanaji mikopo kwenda sekta binafsi na hivyo kutofanikisha miradi mingi ya sekta hiyo iliyotarajiwa.

Taasisi hizo za fedha zilikumbwa  na ongezeko la mikopo isiyolipika yaani chechefu (NPL) ambayo pamoja na sababu nyingine za wafanyabiashara ilichangiwa na hatua kadhaa zilizochukuliwa na serikali kudhibiti matumizi yake na vilevile kukosa kuwalipa wadeni wake wa ndani kwa wakati. Tatizo hili linaonekana kuwa sugu.

Idadi ya wafanyakazi hewa walioondolewa ambayo ni sawa na asilimia 2.3 ya wafanyakazi 435,000 wa umma, walikuwamo waliokopa kutoka kwenye mabenki 58 yaliyopo hivyo kuchangia ongezeko la uchechefu na kufikia asilimia 9.5 Disemba mwaka jana.

Kutokana na uhalisia huo, benki zilichukua hatua ili kubana mikopo kuepuka kushindwa kujiendesha.

Mabenki yalipunguza mikopo kwa sekta binafsi kutoka asilimia 26.5 hadi asilimia 2.5 na hivyo kupunguza shughuli za benki hizo  pamoja na faida yake kwa miaka miwili mfululizo na kuzigusa hata miamba ya sekta hiyo ikiwamo CRDB, NMB na NBC zenye zaidi ya asilimia 40 ya rasilimali za benki zote na wateja wengi zaidi.

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker alisema uamuzi wa serikali kuelekeza fedha nyingi kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo utakuwa na faida mtambuka kwenye sekta nyingi za uchumi na kipato cha wananchi kwa ujumla.

Anasema kulikuwa na changamoto kadhaa mwaka huu, lakini mwakani mambo yatakuwa tofauti na benki imejiimarisha vilivyo na tutaendelea kutoa gawio kwa serikali.

Miongoni mwa miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa na serikali ni kuifufua Kampuni ya Ndege (ATCL), ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), uboreshaji wa viwanja 8 vya ndege na usambazaji wa umeme vijijini. Serikali imeahidi kuwa kuanzia Januari mwakani, kutakuweko miradi mikubwa mingine ya serikali ikiwamo uboreshaji wa bandari na ujenzi wa eneo maalumu la biashara Bagamoyo itaanza.

Serikali imejiimarisha katika miundombinu ya fedha zake na sasa iko tayari kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwani imeonekana imeokoa mabilioni ya fedha kwa kuimarisha mifumo yake ya mapato na malipo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles