25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

NDUGU WA KAMUSOKO AITANGAZIA VITA YANGA

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Singida United, Michelle Katsavairo, amesema atahakikisha anapambana ili kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga, utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katsavairo, ambaye ni raia wa Zimbabwe kama ilivyo kwa Thaban Kamusoko na Donald Ngoma wanaoichezea Yanga, alisema anaamini watautumia vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa kuibuka na ushindi.

“Hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza kukutana na Yanga, hata hivyo, niliwaangalia kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Simba, walicheza vizuri, lakini upande wetu sisi tunahitaji ushindi kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” alisema.

Alisema yeye binafsi amejiandaa kuifunga Yanga kama atapata nafasi ya kucheza baada ya kukosa pambano la kirafiki kati ya timu hizo wakati wa maandalizi ya msimu mpya.

“Nafahamu mchezo utakuwa mgumu kwani kila timu inahitaji matokeo, ukizingatia tumetoka sare kwenye mechi iliyopita kama ilivyokuwa kwa wapinzani wetu, lakini tutahakikisha tunapata pointi tatu,” alisema.

Mshambuliaji huyo amefanikiwa kuifungia Singida United mabao mawili katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kutua kwa  mkopo akitokea Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

 

 

Singida United inashika nafasi ya sita  katika msimamo wa ligi hiyo sawa na Tanzania Prisons iliyoko nafasi ya tano kutokana na wastani wa mabao ya  kufunga na kufugwa, ikiwa imejikusanyia pointi 13 baada ya kushinda mechi tatu, sare nne na kupoteza mchezo mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles